GET /api/v0.1/hansard/entries/390162/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 390162,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/390162/?format=api",
    "text_counter": 89,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "September 18, 2013 SENATE DEBATES 14 Sen. (Dr.) Machage)",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika, asante, kwa kunipa nafasi hii ili nimuunge mwenzangu katika pendekezo ambalo amelitoa kwa Seneti hii kupitia Hoja hii. Yeye mwenyewe kwa fikira zake ameangalia na kunukuu Kipengele cha Kwanza cha Katiba ya Kenya, mstari wa nne, Kipengele cha Sita, mstari wa pili na pia kibandikizo cha Katiba, Sura ya Sita na Kipengele cha 15, mstari wa pili. Bw. Spika, hili sio wazo lake tu bali ni la Kikatiba. Wale watakaopewa kazi hiyo wanafaa wawe wameelimika ya kutosha kwa utawala wa mgambo. Ni kweli kabisa kwamba Katiba mpya imetoa sehemu mbili tu za utawala, Serikali ya taifa na serikali za ugatuzi. Huenda mawazo ya elimu ambayo watawala wetu wanayo wakati huu hayatoshi. Ni lazima Serikali ya Jubilee iliyopo sasa ielewe na kukubali kwamba sehemu za utawala wa nchi hii ni mbili tu Kikatiba, ingawa wameweka kibandikizo ambacho hakikubaliki kikatiba, kuwatafutia kazi tu wale waliokuwa wakuu wa mikoa wakati huo. Hatukubaliani na hilo wazo lao. Tuna sehemu mbili tu za Serikali kulingana na Katiba. Bw. Spika, kwa hivyo, pendekezo la mwenzangu juu ya hii, haitoi nafasi ya mawazo ya kufundisha wale wametunukiwa utawala kwa hiyo sehemu bandia ya tatu. Ni sehemu mbili tu na hivyo ndivyo Katiba inasema. Tukubali kwamba hili ni wazo ambalo lilikuja miaka 58 zilizopita. Wakati huo tulikuwa na kituo kimoja cha kufundisha utawala, yaani, KIA. Bunge hili ilipitisha Hoja hapo awali kwamba tuwe na chuo kikuu kwa kila makao makuu ya kaunti. Mwenye Hoja hiyo anafaa kufikiria kama ingekuwa vizuri kugeuza na kusema kwamba kila chuo kikuu ambacho kitaidhinishwa kiwe na sehemu ya kufundisha mawazo haya ya utawala mpya, ili Hoja hii ambayo imependekezwa na Sen. Wako iingie. Itakuwa jambo la manufaa, kheri na haki kama tunapoanzisha vyuo vikuu hivi tuwe na sehemu ambazo zimeundwa kwa ajili ya kufundisha elimu ya utawala wa mgambo. Tukifanya hivyo, tutakuwa tunapiga hatua mbele. Bw. Spika, hata hivyo, kile ambacho mwenzangu ameomba labda ni upanuzi wa chuo ambacho tayari kipo, ili kiweze kumeza---"
}