GET /api/v0.1/hansard/entries/390188/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 390188,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/390188/?format=api",
"text_counter": 115,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Hassan",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 431,
"legal_name": "Hassan Omar Hassan Sarai",
"slug": "hassan-omar-hassan-sarai"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda. Baadhi yetu tumeamua katika zamu hii tuendeleze Lugha ya Kiswahili ili tuijenge. Mwanzo kabisa nimesimama hapa kuunga Hoja hii mkono ambayo imeletwa na Seneta wa Busia. Yeye ni Mwenyekiti wa Kamati yetu ya Legal Affairs and Human Rights. Kuna watu walisema wakati wa kupigania Katiba mpya kwamba wao wangepiga “ndio.” Walipoulizwa kwa nini wanaipigia Katiba “ndio,” wakasema ni kwa vile Sen. Wetangula ameisoma na akasema ni sawa. Wakati huu tuna Hoja ambayo imewasilishwa hapa na Sen. Wako. Hoja hii ninaiunga mkono kwa sababu ni well though through kama vile Sen. Kagwe alivyotamka. Jambo la pili, Bw. Spika wa Muda, sisi hapa Kenya tumezoea kazi za ukarabati katika kila kitu. Tunajifanya sisi tunajua kila kitu zaidi kuliko watu wengine. Sijui kama hata wewe, Mwenyekiti, ni mmoja wao? Ukiharibikiwa na mfereji wa maji, unaufungua wewe mwenyewe. Wewe unakuwa ni fundi wa mifereji ya maji. Ukiharibikiwa na stima nyumbani, unaitengeza ile swichi wewe mwenyewe. Mara nyingi watu wetu wamekufa kutokana na mshituko wa umeme. Tukiuliza kilicho sababisha kifo, tunaambiwa alifungua soketi ya stima bila kujua ina waya tofautitofauti kama vile earth na live . Anakufa ovyo kwa sababu hataki kumpa kazi fundi wa stima Kshs200."
}