GET /api/v0.1/hansard/entries/390190/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 390190,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/390190/?format=api",
    "text_counter": 117,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Kwa hivyo, huwezi ukawa unajua kila kitu. Kila kazi ina fundi wake. Unaweza kuona hii kazi ya kuweka hivi vitambaa vya “Senate Majority Leader ” labda ni kazi ya rahisi. Lakini ile siku utajaribu kuiweka wewe wenyewe, utaona ni kazi ngumu. Kwa hivyo, usimwone mwenzako akifanya kazi ukafikiria ni kazi rahisi kabisa. Usije ukaona Spika wetu, Bw. Ethuro, akimachi hapa ukaona ile machi yake ukadhani ni rashisi. Labda wewe ukipewa fursa umachi hivyo, pengine hautaweza. Kwa hivyo, kila mtu yuko na ujuzi wa kazi yake na ni vizuri kuuheshimu. Bw. Spika wa Muda, ugatuzi wetu hauwezi kuwa wa ukarabati. Kila mtu hawezi kujifanyie analotaka kiholela holela. Wewe hauwezi kuwa mtaalamu wa kila jambo. Kuna watu wanaotaka ugatuzi na kuna wengine wanaoupiga vita. Wale wanaouunga mkono pengine hawana maarifa ya kuuendeleza. Kwa hivyo, lazima tujenge hii taasisi ya kuhakikisha kwamba tuko na maarifa, na watu wanapatiwa uwezo. Kila wakati suala la ugatuzi linapotajwa, watu wengine wanasema hawana uwezo. Tumepatiwa wafanyakazi waliokuwa katika Serikali za Mitaa na wao bado wako na fikra za mitaa. Wanafikiria hii serikali ya kaunti bado inaongozwa na meya wa zamani. Wanataka kuendeleza zile sera za wizi na ufisadi. Hii ndio maana kila wakati serikali zetu za ugatuzi zinapata shida. Watu wengi kule mashinani wanaongozwa na fikira za kizamani. Hata mimi wakati mmoja nilipokuwa nimeingia kama Kamishna wa Tume ya Kitaifa ya Kutetea Haki za Kibinadamu, nilienda nikapata watu tayari wameganda. Watu hawa waliletwa na wale makamishna waliokuweko kabla yetu. Nilipoenda pale, niliwaambia kuwa “haya ndio maarifa yangu ya kufanya mambo haya.” Lakini wao wakaniambia kuwa aliyenitangulia alifanya mambo yake tofauti kabisa. Mimi nikawaambia kuwa kuna mkuu mpya wa polisi mjini; there is a new sheriff in town . Kwa hivyo, sasa, yule mkuu mpya wa polisi ni ugatuzi. Hatuwezi kuendeleza ugatuzi bila ya ile taaluma inayostahiki. Hii ndio maana ninaunga mkono Hoja hii ya Sen. Wako. Seneta Amos Wako ni mtu aliyebobea katika masuala ya kiserikali na kisheria. Yeye anajua kuwa lazima kuwe na taasisi itakayoweza kuwapatia watu uwezo wa kufanya kazi kama hii. Bw. Spika wa Muda, ni lazima taasisi zetu nyingi pia ziwe na utafiti. Wajua katika hii nchi, hatujaweza kuweka mkazo katika masuala ya utafiti katika maendeleo yetu; the role of research in modernization . Lazima tuwe na msingi mkubwa katika masuala ya utafiti. Kwa hivyo, hii isiwe kama vile waalimu wetu katika vyuo vikuu na vyuo vyetu wanavyofanya; mtu aliandika silabasi miaka mitatu iliyopita, kazi yake ni kuja na kuzisoma tu hizo notes zake. Wanafunzi hunukuu maandishi hayo moja kwa moja ili wafaulu mitihani yao. Tuko na waalimu kama hao. Lazima kila siku tufanye utafiti. Ninajua Bw. Spika wa Muda, katika maisha yako, wewe ni mtafiti wa taaluma. Hili linamanisha kuwa kila siku lazima unasoma upya na unapata maarifa mapya. Kwa hivyo, lazima tuhakikishe kuwa kila siku, tunafanya utafiti. Sen. (Prof.) Lesan yuko hapa na anajua the role of research katika maisha yetu. Taasisi hizi zitatusaidia kupata maarifa mapya kila siku na kuhakikisha kwamba tunaimarisha sera yetu ya ugatuzi. Sen. Wako alisema kuwa kuanzisha taasisi hii ni lazima kwa Serikali yetu. Serikali haina hiari ili kutekeleza Hoja hii. Sisi tumezoea ile serikali au siasa ya “baba na mama;” ambapo kila wakati tunaiomba Serikali kufanya hili na lile. Katika Hoja hii Serikali ya Kitaifa imeshurutishwa kisheria kuwa lazima isaidie serikali zetu za ugatuzi ili kuziwezesha kuendeleza ratiba zake. Kwa hivyo, hii ni amri ya kikatiba. Sisi kama Seneti ambayo ni Bunge kuu la Taifa ya Kenya, linatoa mwongozo maalum kwa Serikali"
}