GET /api/v0.1/hansard/entries/390194/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 390194,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/390194/?format=api",
"text_counter": 121,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": ". Hili ni Jumba la hekima. Kazi yetu ni kufikiria lile jambo zuri kwa taifa letu. Na sisi tunaleta hapa hilo jambo, linapendekezwa, linakubalika kwa sauti moja na tunalitekeleza kwa kauli moja. Bw. Spika wa Muda, Hoja hii ikipitishwa tunataka kuona taasisi hii imeanzishwa mara moja. Taasisi hii lazima ibuniwe moja kwa moja. Kwa hivyo, tunatakiwa pia tutoe mwongozo wa lini taasisi au Hoja hii itatekelezwa na Serikali ya Kitaifa. Bw. Spika wa Muda, ni jambo la kuhuzunisha kuwa tulipitisha Hoja hapa kuwa madeni yote ya serikali zetu za kaunti yafutiliwe mbali. Lakini mpaka leo hatujajua hatua iliyochukuliwa na Serikali ya Kitaifa. Kwa hivyo, yatakikana tuiambie serikali yetu ni lini sisi tunataka wao waanzishe au waweke jiwe la msingi la taasisi hii ya masuala ya ugatuzi. Bw. Spika wa Muda, kama kweli tunataka ugatuzi wetu uimarike na ufaulu, lazima tuwe na watu ambao wanauelewa vizuri kwa kuangalia zile sera za ugatuzi wakilinganisha serikali za ugatuzi katika ulimwengu mzima. Wanapochanganua sera hizo ni lazima watuelekeze kuyaiga mambo yote mazuri ya ugatuzi. Pia sisi kuambatana na fikra na uchambuzi wetu, tutachukua yaliyo mazuri kwetu. Ni lazima tupate watu ambao wako na uwezo wa kutekeleza ahadi zote za ugatuzi. Bw. Spika wa Muda, pia ni kuwashurutisha ama kuwasihi magavana wetu washinikize na wahakikishe kwamba wameleta watu wenye uwezo wa kutekeleza ugatuzi. Wengi wao wamechukua watu kutoka katika ngazi mbalimbali za utawala wa kaunti zetu. Je, watu ambao hawana ujuzi wa ugatuzi, watautekelezaje? Bw. Spika wa Muda, nafikiria katika fikra yangu, Sen. Amos Wako, ambaye ndiye mwenye kubuni Hoja hii alikuwa na wazo kwamba kupata mtu mzuri inaenda sambamba na kuwa na ufadhili mzuri. Ukilipa vizuri utapata mtu mzuri. Hauwezi kuchukua mtu kwa pesa nane na ukafikiri kwamba utapata matokeo kama yale ambayo tunapata kutoka kwa kampuni za kibinafsi. Kwa hivyo lazima tuimarishe mapato katika kaunti zetu ili tuweze kulipa wafanyakazi wa kaunti kwa njia nzuri ndio tutapata watu wazuri ambao watakuza uchumi wetu. Hata hapa katika Serikali yetu ya kitaifa, baadhi ya wale ambao waliweza kukuza uchumi wetu ni wataalamu wakubwa kutoka World Bank na economists wakubwa kama Bw. Thuge. Waliletwa hapa na kuhusishwa katika kukuza uchumi wetu kwa kutoa fikra na mbinu za kutekeleza ile ahadi ya kuboresha uchumi. Kwa hivyo kama kweli tunataka wafanyakazi wa kaunti ambao wataweza kuhudumia taifa hili kwa kujitolea, lazima pia tuwaweke katika hali ya utulivu. Ikiwa utalipa mtu Kshs20,000 nakuhakikishia kwamba muda mwingi atautumia katika wizi na kutafuta mapato mengine hapa na pale. Kwa hivyo, hatuwezi kumlaumu. Ikiwa wewe unalipwa millioni moja na unamwambia afanye bidii kama wewe na pia apende kuwa Mkenya--- Lazima upende kuwa Mkenya kama uko na mali. Sisi tunawaomba muunge mkono Hoja hii ili kuhakikisha kwamba tumetekeleza ahadi zetu za ugatuzi."
}