GET /api/v0.1/hansard/entries/390468/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 390468,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/390468/?format=api",
"text_counter": 233,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Boy Juma Boy",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 758,
"legal_name": "Boy Juma Boy",
"slug": "boy-juma-boy"
},
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, ningependa kumshukuru Sen. Anyang’-Nyong’o kwa kuileta Hoja hii. Ningependa kwanza kuichambua Hoja hii. Hoja hii yasema nini? Hoja hii yataka vyama vya kisiasa vipewe ufadhili. Hoja hii haisemi kwamba Chama Cha Jubilee, ODM ama chama kingine kipewe ufadhili. Kinachoonekana katika Hoja hii ambacho ni cha muhimu ni swala la ufadhili ama hela kutoka kwa Serikali. Vyama vinafaa kupewa hela. Je kuna umuhimu wa vyama kupewa hela? Umuhimu upo. Umuhimu huu ni upi? Tunaijua maana ya demokrasia. Tukitaka mambo yafanyike kulingana na Katiba, ni lazima tutumie fedha. Tutaimarisha demokrasia vipi kama vyama vyetu ni masikini hohe hahe? Hoja hii inataka tuwe na ufadhili. Hii ndiyo sababu tunasema Bwana huyu kweli ni Profesa. Mkisikia watu wengine wakiitwa maprofesa, msije mukasema ni uongo. Ni ukweli anafaa kuitwa Profesa. Hii ndiyo sababa anaitwa Sen. (Prof.) Anyang’-Nyong’o. Huu uprofesa ndio umemfanya akaona kwamba vyama vya kisiasa vina shida. Twakubaliana, bila pingamizi yoyote kwamba ni kweli, vyama vina shida. Shida kubwa iliyo katika vyama vyetu ni shida ya mishahara. Wafanyikazi ambao wameajiriwa na vyama wanahitaji mishahara. Hawali upepo. Ili kuhakikisha mishahara inapatikana, ni lazima fedha zipatikane. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}