GET /api/v0.1/hansard/entries/390470/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 390470,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/390470/?format=api",
    "text_counter": 235,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Kuna Rais mmoja wa zamani wa Tanzania, Rais Nyerere, aliyesema kwamba hakuna demokrasia itakayopatikana kama hatuna vyama vinavyojitegemea. Sio mimi Boy niliyesema hivyo bali ni Mwalimu Julius Kabarage Nyerere. Hakuna vyama vya kidemokrasia vitakavyokamilika kama havijitawali kifedha. Ndio maana Hoja hii ina umuhimu sana. Tutazame hali ya vyama hapa Kenya. Tumezoea kwamba vyama ni vyombo vya kisiasa. Kesho na kesho kutwa, kila mtu huwa akiwania chama chake. Kura inapokwisha, vyama huwa havina maana. Demokrasia haiwezi kuendelea hivi. Ni lazima tuhakikishe ya kwamba tumekita mizizi ya kidemokrasia. Demokrasia si kusema tu. Demokrasia ni vitendo na kuhakikisha kwamba yaendelea. Kuendelea kwake ni sisi kuwa tayari kutoa pesa. Hoja hii yasema kwamba sheria ipo. Serikali yaelezwa na kufahamishwa kwamba vyama vipo. Kwa sababu uchaguzi umekwisha, kawaida tunangoja hadi wakati mwingine wa uchaguzi. Huo ndio ukweli wa mambo. Kila mtu ana chama chake; chama baba, chama cha shangazi, chamba mjomba na katika wakati wa uchaguzi, vyote vitafufuka. Hatutaki hivi viwe ni vitu vya kawaida. Hatutaki kuwa na manifesto kila wakati wa uchaguzi. Hatutaki kila mtu awe na manifesto yake. Leo, manifesto tulizokuwa nazo wakati wa uchaguzi ziko wapi? Ziko chini ya makabati ama wapi? Zilitangazwa katika mikutano kubwa. Katika wakati wa uchaguzi, manifesto zinaelezwa kila mahali. Wanasiasa hueleza vijana vile watakapofaidika uchaguzi utakapoisha lakini uchaguzi unapoisha, mambo ya vijana yanasahaulika. Uchaguzi unapokwisha, demokrasia pia huisha. Maendeleo pia hayafanyiki uchaguzi unapokwisha. Haya ndiyo mambo tunayosisitiza katika Hoja hii. Hoja hii yasisitiza umuhimu wa kuwepo kwa fedha. Nimemsikiza vizuri Kiongozi wa Wengi, Sen. (Prof.) Kindiki akisema fedha hazifai kupeanwa na Msajili wa Vyama vya Kisiasa lakini ziombwe kutoka Treasury . Msajili wa Vyama atazigawa vipi kama Treasury haijampa? Mkono wa kulia unasema mambo ambayo mkono wa kushoto hauoni.Msajili wa Vyama ndiye anayefaa kuzigawa pesa na anajulikana. Bi. Spika wa Muda, wewe hapa wajulikana kama Madam Temporary Speaker . Akija mwingine mwanamme ataitwa Mr. Speaker . Tunaposema Speaker, tunamaanisha mamlaka. Huu ndio ukweli, upende usipende. Ukitakata kukasirika, basi kasirika lakini huo ndio ukweli wa mambo. Uspika ni kile kiti. Akikaa mwanamme, ataitwa Bwana Spika. Akikaa mwanamke, anaitwa Bi. Spika. Sisi twajua wazi kwamba pesa za Serikali hutoka Treasury . Kama zitagawanywa na Msajili wa Vyama, basi pia zitakuwa zimetoka Treasury . Tunachosema ni kwamba"
}