GET /api/v0.1/hansard/entries/390474/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 390474,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/390474/?format=api",
"text_counter": 239,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Hatufai kuwa tunamwomba Mfadhili wa Vyama ila sheria ipo. Wale walioleta sheria hii kweli walikuwa mabuzuranga ? Mabuzuranga ni watu wasilojua lolote. Waliopanga sheria hii walijua wazi ungefika wakati ambapo vyama vingehitaji hela. Kinachonishangaza ni kwamba ni lazima uambiwe kwamba leo ni Jumatatu bali unajua kwamba leo ni Jumatatu? Hayo ni mambo ya kushangaza. Tukiunga mkono Hoja hii, tunachosema ni kwamba vyama haviwezi kupewa pesa mpaka Hoja zije kutoka Seneti. Naiunga Seneti hii kwa sababu ina wazee na vijana ambao wamekomaa. Iko pia na Spika anayeona mbali. Treasury inafaa kumpatia Msajili wa Vyama pesa ili vyama navyo vianze kutumia pesa hizo. Bi. Spika wa Muda, nimewasikiliza wasemaji wenzangu wakisema kwamba vyama visitumie pesa hizi kwa mikutano. Sasa wewe unasema pesa zisitumike kwa mikutano na hazijakuja? Bi. Spika wa Muda, kwa hayo machache, naunga mkono kikamilifu Hoja hii."
}