GET /api/v0.1/hansard/entries/390642/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 390642,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/390642/?format=api",
    "text_counter": 124,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mbuvi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 80,
        "legal_name": "Gideon Mbuvi",
        "slug": "gideon-mbuvi"
    },
    "content": "Lakini Bw. Spika, siko hapa kumlaumu mtu yeyote yule; huu sio wakati wa kulaumiana lakini kwa sababu maisha ya Wakenya ni muhimu kushinda siasa; usalama wa Wakenya ni kitu cha kuwekewa kipaumbele kuliko mambo mengine yote. Bw. Spika, ningependa kuvipongeza vikosi hivi vingine lakini swali langu liko kwa Kitengo cha Ujasusi kijulikanacho kama National Intelligence Service (NIS) . Walikuwa wapi mambo haya yote yalipokuwa yakipangwa? Niko ndani ya Serikali na nina imani na Serikali ya Rais Uhuru Kenyatta na Naibu wake, William Ruto. Lakini katika mambo ya uongozi lazima tuwe serious na maslahi na usalama wa Wakenya. Haya mambo ya kushambuliwa yamefanyika Garissa, Mandera na mahali kwingi katika nchi yetu ya Kenya. Haya si mambo yamefanyika jijini Nairobi peke yake. Mashambulizi haya yote yanapofanyika, Idara ya Ujasusi, ikiongozwa na Bw. Gichangi huwa wako wapi ama wakifanya kazi gani?"
}