GET /api/v0.1/hansard/entries/390751/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 390751,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/390751/?format=api",
    "text_counter": 233,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika. Ningependa kuungana na wenzangu kutoa rambi rambi zangu kwa Wakenya waliopoteza maisha yao na hasa taifa nzima. Nimeshangaa sana kuona ya kwamba, vile tunavyozungumzia mambo haya, nchi yetu imesimamiwa na Wakenya. Juzi tulishangaa tuliopoona mlanguzi wa madawa ya kulevya akipelekwa kwao kule Nigeria na baada ya wiki tatu, huyo mlanguzi alipatikana katika nchi yetu akiwa ametengenezewa makaratasi ya kuingia nchini na Wakenya wenyewe. Jambo lilioko mbele yetu ni kwamba nchi ya Kenya imepigwa na kama wananchi, tunataka kuungana pamoja ili tulinde taifa letu. Ningependa kusema wazi wazi kwamba tunaweza kutofautiana hapa kama wanasiasa lakini akitokea adui, watu wasifikirie kwamba watatugawanya. Hiyo haiwezekani."
}