GET /api/v0.1/hansard/entries/390752/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 390752,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/390752/?format=api",
"text_counter": 234,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Adui amefika kwa nyumba na ni jukumu la Wakenya kuungana pamoja na kumtoa. Hawa maharamia wanatuchukia na taifa letu kwa sababu tumeingia nchi ya Somalia. Hatukuingia nchi ya Somalia kwa sababu tulikaribishwa ama kulikuwa na mali ambayo Kenya ilitaka kuchukua kutoka nchi ya Somalia. Hakuna chochote cha thamani Wakenya wanaweza kuchukua kutoka nchi ya Somalia. Lakini wao wameingia ndani ya nyumba yetu na kuanza kuchukua watoto wetu. Walianza kuchukua wageni hapa nchini na kuwapeleka kwao. Ilikuwa ni kawaida ya taifa nzima kumfuata yule adui na kumfunza adabu. Kwa hivyo, kama wanafikiri watakuja kutuchokoza ili watuumize, inafaa wafahamu kwamba, taifa hili liliungana kumuondoa mkoloni na tutaungana kabisa ili tuhakikishe ya kwamba amani ya nchi hii imelindwa."
}