GET /api/v0.1/hansard/entries/390755/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 390755,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/390755/?format=api",
    "text_counter": 237,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Vile Sen. Mbuvi amesema hapa – na ninarudia – hakuna kitengo ambacho hakisimamiwi na Mkenya. Kwa hivyo, kama mwenye kuongoza idara ya kuchunguza na kufahamu ni nani anayeingia na kutoka nchini amelala, ni jukumu la Wakenya kumwondoa na kuweka Mkenya mwingine kufanya kazi hiyo. Sisi hatuwezi kuhatarisha maisha ya watu ovyo ovyo. Unawezaji kuwa nahodha wa meli na inazama na ukose kuulizwa kazi yako ni nini? Kama hutaki kuulizwa, usiwe nahodha wa hiyo meli. Inafaa ukae kando ili iendeshwe na mwingine halafu ikizama, yeye aulizwe. Watu 15 ambao wamejihami wakiingia katika shopping mall, hili ni jeshi nzima."
}