GET /api/v0.1/hansard/entries/390819/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 390819,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/390819/?format=api",
    "text_counter": 301,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chiaba",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 3,
        "legal_name": "Abu Mohamed Chiaba",
        "slug": "abu-chiaba"
    },
    "content": "Asante Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii. Nakushukuru kwa sababu umeniona. Nimekuwa nikisimama mara nyingi lakini macho yako hayakuniona. Nakushukuru sana kwa kuniona ili niweze kuungana na wenzangu kutoa hisia zangu juu ya Hoja hii. Naishukuru Seneti kwa kutenga kipindi hiki cha adhuhuri ili kuzungumzia mambo muhimu yaliyotokea katika nchi yetu siku tatu zilizopita. Yale yaliyotokea ni mambo ya kulaaniwa na kila binadamu. Watu wote wanakilaani kitendo hicho kilichofanyika kule Westgate Mall bila kujali kama mtu ni Muislamu, Mkristu, Budhist au wa dini ile nyinge yoyote. Wale waliotenda kitendo hicho si Waislamu. Mimi kama Muislamu nimesoma dini kwa zaidi ya miaka 30. Bado sijahitimu katika masuala ya kidini lakini sijaona mahali ambapo magaidi wanatambulika. Hakuna nafasi ya magaidi kutambuliwa na Mwenyezi Mungu. Ninajua na nina imani kwamba Bibilia haitambui ugaidi wala kitendo cha ugaidi. Kitendo kilichofanyika juzi katika Jumba la Westgate kimesababisha vifo vya Waisilamu, Wakristu, Wahindi na wasiokuwa na dini. Jirani yangu mita kumi kutoka kwangu ni Muhindi. Yeye hana dini lakini nilienda kumpa pole kwa sababu mtoto wake ambaye alikuwa aolewe karibuni alifariki katika mkasa huo wa Westgate Mall. Nilienda kumzika Msomali ambaye ni Muislamu katika Makaburi ya Langata. Yeye pia aliuawa katika mkasa huo. Pia Wakristu waliathirika sana katika mkasa huu. Ningependa watu ambao wanajua kuhusu dini zote waniambie kama dini ya magaidi ni ya Kiislamu, Kikristu au dini ile yoyote. Hawa magaidi hawana dini yao wala hawatambuliwi na dini yoyote. Kwa hivyo, magaidi wanapofanya kitendo kibaya huwa hawajaelekezwa na Mwenyezi Mungu. Mimi ninaamini ya kwamba badala ya magaidi kwenda peponi, watakwenda motoni. Yafaa sisi sote tusimame imara kulinda nchi yetu na dunia nzima. Hatuna uhakika lakini tunaambiwa magaidi hawa wametoka Amerika, Canada na Uingereza. Kuna uwezekano kwamba kati ya magaidi hawa kuna Waislamu na Wakristu. Magaidi hawana nafasi katika dini yoyote. Nimesoma aya ya Kurani ambapo Mwenyezi Mungu anasema: “Hakuna mtu yeyote aliye na haki ya kutoa roho ya binadamu isipokuwa Mwenyezi Mungu.” The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}