GET /api/v0.1/hansard/entries/390877/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 390877,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/390877/?format=api",
    "text_counter": 359,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mositet",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 608,
        "legal_name": "Peter Korinko Mositet",
        "slug": "peter-korinko-mositet"
    },
    "content": "Bi. Spika wa Muda, siasa ambayo tumezoea kama ile ya Referendum na maneno mengine huwa inatugawanisha, lakini jambo kama hili haliwezi kuigawanya jamii ya Kenya. Hebu na tuzidi kushikana na kuwa kitu kimoja. Bi. Spika wa Muda, mimi ninaweza kusema kwamba ufisadi umesababisha haya mambo. Idara ya uhamiaji inawaruhusu watu kuingia katika nchi ya Kenya kwa uraisi sana. Mimi ningeomba tukiwa viongozi tutafanye lolote liwezekanalo kuwasaka watu wote ambao wameingia hapa nchini kwa njia isiyo ya halali. Kila mwananchi aweze kumtambua jirani yake ambaye si Mkenya ama aliye na tabia mbaya. Sisi tumewakubalia watu wengi kuingia hapa nchi bila vibali maalum. Jambo hili limekuwa likifanyika kwa miaka mingi iliyopita. Wageni wengi wameingia humu nchini bila vibali. Katika Kaunti ya Kajiado, kuna wakati hata watu walikuwa wanasema kwamba siku hizi ikiwa wewe ni mwalimu wa Kiswahili, uende Kajiado ili uwafundishe wageni lugha hii jioni. Kuna wageni wengi ambao waliingia katika nchi hii bila vitambulisho na hawajui neno moja la lugha ya Kiswahili au Kiingereza. Lakini utaona ya kwamba raia wa Kajiado wanawajua. Hiyo inamaanisha kwamba hata walinda usalama wetu wanajua lakini kwa sababu ya kupokea hongo kutoka kwao, hawana shughuli nao. Wanawacha nchi iharibike na kuwa katika hatari sana."
}