GET /api/v0.1/hansard/entries/390881/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 390881,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/390881/?format=api",
    "text_counter": 363,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwakulegwa",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 101,
        "legal_name": "Danson Mwazo Mwakulegwa",
        "slug": "danson-mwazo"
    },
    "content": "Magaidi ni maajenti wa shetani. Na kama unaenda kupigana na shetani, ni lazima ummalize kwa sababu ukimwaacha, atakumaliza wewe. Sisi tukimuona nyoka, tunasema ni shetani. Nyoka ukimuua, ni lazima umgonge kichwa. Kwa hivyo, ni lazima tuwe na mbinu ya kupambana na magaidi hawa. Tusilaumiane kidini au kikabila. Inafaa tuwe na sheria mpya ambazo zitaongoza wale wanaofanya kazi katika mipaka, viwanja vya ndege na bandari ili tufahamu ni mtu yupi anayeruhusiwa kuingia nchini. Pili, akiingia nchini Kenya tutamfuata vipi ili tujue ni vitendo gani anavyofanya ndani ya nchi. Tumeshindwa na mataifa majirani wetu. Hata ukienda Namanga, ukiongea Kiswahili, maafisa wa usalama watakutambua kama Mkenya na watakuuliza maswali fulani. Hapa nchini Kenya, mtu anaweza kufika katika kituo cha ndege na kupandishwa gari na kupelekwa hadi Kisumu na huku hatujui ni mtu wa aina gani. Inafaa tubadilishe sheria ili kwamba tuanze kuwafuata watu na tujue mienendo yao. Hata kama ni wawekezaji ama watalii, kuna wengine wanaokuja wakijitambua kama watalii na huku malengo yao ni mabaya."
}