GET /api/v0.1/hansard/entries/390882/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 390882,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/390882/?format=api",
    "text_counter": 364,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwakulegwa",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 101,
        "legal_name": "Danson Mwazo Mwakulegwa",
        "slug": "danson-mwazo"
    },
    "content": "Bi. Spika wa Muda, tusije tukaweka lawama, lakini ninajua tutazungumza hapa na kusema kwamba, kama mtu amekaa kwa ofisi kwa miaka mingi, labda uzoefu na maarifa yamepungua, inafaa tufanye mabadilikio. Let us change the management . Katika usalama wa Kenya tunafaa kubadilisha jambo gani ili Kenya ithibitiwe kama nchi huru ili kwamba yaliyofanyika juzi hayatatendeka tena ? Ninaomba Mungu sana. Mimi nilikuwa pale na baada ya kuondoka, kwa muda wa dakika kumi nikienda Village Market, nilipigiwa simu kuambiwa kwamba pamelipuka. Ninapigia Mungu wangu asante na wale mababu zangu walioenda mbele. Kama ningekuwa pale, labda leo mngekuwa mnaomboleza. Lakini tuseme kwamba yaliyotokea iwe ni funzo. Tusilaumiane na tusije tukasema kwamba fulani hajafanya makosa. Kosa ni kosa. Lakini kurudia kosa, ndio kosa zaidi. Kama yamefanyika, tuyatatue."
}