GET /api/v0.1/hansard/entries/390904/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 390904,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/390904/?format=api",
"text_counter": 386,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mbura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13153,
"legal_name": "Emma Mbura Getrude",
"slug": "emma-mbura-getrude"
},
"content": "Bi. Spika wa Muda, ningependa kusema kwamba yule ambaye alihusika na kisa cha kigaida cha Twins Tower huko Marekani, mkewe ndiye yuko katika vyombo vya habari; anaitwa Samantha. Yeye ndiye mastermind wa kitendo cha Westgate Mall. Ametoa habari kwa facebook akisema kwamba hivi karibuni ataungana na mumewe. Mumewe alikufa kwa hivyo inamaanisha kwamba anaenda kufa. Kwa hivyo, huyo ni mwanamke amejihami, na vyombo vya habari vimetangaza hivyo. Je, Serikali ya Kenya inajipanga vipi kukabiliana na matamshi ya huyu mwanamke? Ningependa kuiomba Serikali yetu ya Kenya isilaumu Wizara ya Usalamu. Mwanadamu alimshinda Mungu akili. Katika Bustani la Eden Mungu aliwaumba Adamu na Hawa na akawapa masharti. Hata hivyo, shetani aliwashinda nguvu na wakamgeuka Mungu. Mungu Hakuwaua lakini aliwafukuza. Mwanadamu ni mtu aliye na akili. Viongozi kama hao hubabaika dereva anapoindesha kwa kasi bila kujiuliza kama dereva huyu angependa kufa."
}