GET /api/v0.1/hansard/entries/391040/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 391040,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/391040/?format=api",
"text_counter": 114,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Hoja hii ni muhimu kwa sababu inaguzia swala la ugatuzi. Seneta ambaye ameleta Hoja hii amelenga pande mbili. Pande hizi ni kaunti na Serikali kuu. Serikali kuu inafaa kuhakikisha ya kwamba kaunti zote zimeunganishwa na mtandawazi huu. Kwa hivyo, hapo ni lazima tumsifu mwenye kuleta Hoja hii. Alijua wazi kwamba serikali za kaunti hazina uwezo; ndio maana akasema kwamba Serikali kuu ihakikishe kwamba makao makuu ya serikali ndogo yameunganishwa. Tukifanya hivyo mawasiliano yetu yatakuwa mazuri. Kwa mfano, mkuu wa wilaya anaweza kuwasiliana na Serikali kuu kupitia mtandao. Kutokana na hali hii, hebu tuangalie hali yetu vile ilivyo sasa. Wakati huu, mapato yote ambayo yanatoka katika serikali ya wilaya ni lazima yapelekwe katika hazina kuu ya Serikali. Watu wa wilaya wakitaka kutumia pesa hizo ni lazima wapate ruhusa kutoka hazina kuu ya Serikali. Kwa hivyo, mambo haya yanaweza kuunganishwa na mtandawazi. Hakutakuwa na haja ya kuandika barua. Wahusika watakuwa wakikaa kwenye tarakilishi zao na kuwasiliana moja kwa moja na Waziri wa Fedha katika Serikali kuu. Kazi itafanyika mara moja. Haina haja mtu kusafiri kutoka Kaunti ya Turkana ili kupata kibali cha matumizi huku Nairobi. Wakati wa kufanya hivyo umepita. Zaidi ya miaka 50 ni lazima tubadilishe vile tunafanya mambo hapa. Bi. Spika wa Muda, kati ya kaunti 47 katika nchi yetu ni kama 20 ambazo zimeunganishwa na mtandawazi huu. Moja kati ya kaunti hizo ni ile ya Kwale. Kaunti hii ina matatizo. Kwale ina ufuo wa bahari ambapo kuna mahoteli. Kwa hivyo, mtandao huu umeletwa na ukapelekwa mpaka hotelini kwa sababu huko ndipo kuna matumizi mazuri. Ni kule ndipo wakubwa huenda kulala. Lakini kule kwa mlima ambapo wanakaa wananchi hohehahe na walalahoi au watu wa kawaida, mtandawazi haujafika. Mahali ambapo gavana anaishi hakuna tarakilishi. Mtandawazi huu umeunganishwa katika hoteli ya Leisure Lodge, Diani na Neptune. Mambo haya hayafai. Huu ni ubaguzi. Tulizunguka na kamati hii mpaka Malindi. Kule wenyeji ni Wagiriama. Hata hivyo, wengi wa wakaazi wa hapo ni Waitaliano. Hapa kuna tarakilishi lakini Kilifi ambapo kuna walalahoi wengi hukuna mambo haya. Hii ndio sababu mwenye kuleta Hoja hii alisema kwamba mambo haya yafanywe na Serikali kuu. Ndio maana mwenye Hoja alifafanua kwamba anahimiza Serikali kuu ihakikishe kwamba serikali za ugatuzi The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}