GET /api/v0.1/hansard/entries/392037/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 392037,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/392037/?format=api",
    "text_counter": 50,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Bw. Spika, nasimama kuunga mkono Hoja hii. Tumeingia katika muundo mpya wa Serikali na matumaini yetu kama viongozi ni kuona kwamba chanzo, mwenendo na mipango yote tunayofanya inawasaidia wananchi wote. Bw. Spika, waliozungumza kabla yangu wametaja mambo fulani. Ninataka kuyazungumzia mambo hayo kwa mapana na marefu ili tusielekeze lawama kwa Serikali kila mara. Leo Katiba yetu iko wazi sana. Tulibuni vipengele vingi sana katika Bunge letu la Kumi ambavyo vitasaidia serikali za ugatuzi. Bw. Spika, nikiangalia Hoja hii iliyoletwa na Sen. Elachi ni muhimu sana. Shirika la TA halina shida yoyote ila ni Serikali inayoleta matatizo. Chanzo cha matatizo haya ni magavana wetu. Hata hivyo, mimi sitaki kuwalaumu magavana, ila tu nataka kuwashauri. Katiba yetu inaruhusu Kenya moja. Tuna umoja wa Wananchi wa Kenya. Lakini ukiangalia kwa undani sana, utaona ya kwamba magavana wameweza kuchukua majukumu yao kwa nguvu sana. Hawataki kusaidiana na viongozi wengine. Bw. Spika, tumeshuhudia wafanyakazi wa Serikali wakitimuliwa kutoka ofisini na Gavana wa Machakos. Ofisi zao zimefungwa pasipo sababu maalum. Jambo hili linapofanyika, ofisi zinabaki bila mtu wa kutoa huduma kwa watu wetu. Wafanyakazi wanafutwa kazi ovyovyo bila sababu yoyote. Wakenya wako na haki ya kufanya kazi popote hapa nchini. Ni jukumu la Serikali kuwapa watu wake nafasi za kazi. Hakuna Mkenya kuanzia Mheshimiwa Rais hadi mtu wa kawaida aliye na uwezo wa kufuta mtu kazi bila sababu maalum. Hakuna kiongozi aliye na uwezo wa kufunga ofisi ya mfanyakazi yeyote wa Serikali. Katiba inahitaji sisi sote kuheshimiana. Ni lazima sisi sote tuheshimu haki za watu wetu, wawe matajiri au masikini. Katiba yetu imetupa haki sawa. Lakini magavana wanachukulia jambo hili kama ni muundo wa serikali za kaunti. Bw. Spika, tabia yao ni kama wameingia na kasumba ya kupindua Serikali na kudhani kuwa wao ndio wenye mamlaka ya kusimamia nchi nzima. Tusipotahadhari nchi hii itagawanywa katika misingi ya kikabila na magavana wetu. Ni lazima wajue ya kuwa kila Mkenya ana haki kufanya kazi katika kaunti yoyote. Ikiwa wewe ni Mkamba, unawezafanya kazi katika kaunti ya Kirinyaga. Ni aibu iliyoje kuona kuwa kuna magavana wengine ambao wanapenda kuitwa kwa jina maalum la “mtukufu”. Wengine wanafikiria kuwa wana mamlaka sawa na mheshimiwa Rais. Wamelewa na kasumba ya uongozi. Hii ndio maana wanafuta kazi wafanya kazi wa Serikali bila kujali watakwenda The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}