GET /api/v0.1/hansard/entries/392039/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 392039,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/392039/?format=api",
    "text_counter": 52,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "wapi. Kwa hivyo, wafanya kazi wa Serikali wasifutwe kazi bila sisi kuja na sera maalum. Hatutaki kuona wananchi wetu wakiteseka kwa sababu ya uongozi mbaya wa magavana. Bw. Spika, jambo la pili ninalotaka kuliambia Bunge hili ni kuwa ikiwa wataweza kuitoa TA, basi hatua yao ya pili watakayoichukua baada ya hilo ni kuimaliza Seneti. Bw. Spika, magavana hawana haja ya kutawala. Ningependa kusema kwamba Mkenya yeyote ana haki ya kutawala. Hakuna mtu anayekataa. Sen. Orengo amegusia vile vyeo vimegawanywa katika Serikali. Ningependa kutaja jambo moja. Katiba inasema kwamba katika kila uteuzi wa Serikali ni lazima jamii zote za nchi ziwakilishwe ili sura ya Kenya ionekane. Mimi hushangaa sana. Baraza la Usalama la Kitaifa linawakilishwa na watu wa jamii moja. Watu hawa wanaweza kutumia lugha yao katika mikutano yao. Kuna mtu mmoja tu ambaye anastahili kutafsiriwa kinachosemwa katika mikutano yao. Mimi natetea haki ya Wakenya. Ningependa kuona kila jamii imewakilishwa katika Serikali kuu. Kwa hayo machache, ninaunga mkono."
}