GET /api/v0.1/hansard/entries/392201/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 392201,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/392201/?format=api",
"text_counter": 23,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Lesuuda",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13122,
"legal_name": "Naisula Lesuuda",
"slug": "naisula-lesuuda"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika. Naomba nizumngumze kwa lugha ya Kiswahili ili nione kama ujumbe utafika nyumbani ama Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama na Masuala ya Kigeni ataweza kutoa jibu kwa swali ambalo niliuliza kuhusu eneo la Baragoi na Samburu Kaskazini. Niliuliza maswali kadhaa kuhusu swala hili wiki tatu zilizopita. Mwenyekti wa Kamati hii alikuwa ajibu maswali haya Alhamisi wiki iliyopita lakini hakuwepo. Spika aliyekuwa kitini alisema swali hili lijibiwe leo. Bado sioni kama kuna mwanakamati yeyote wa Kamati hiyo. Bw. Spika, hili ni jambo la kuhuzunisha kwa sababu niliuliza swali hili kabla vita havijatokea Baragoi. Kwenye runinga na magazeti, tumekuwa tukiona vita vimeanza tena katika eneo hili. Sijui kama tunachukulia mambo haya kama ya mzaha. Watu kutoka eneo hilo wafaa waambiwe masuala yao hayatiliwi manani."
}