GET /api/v0.1/hansard/entries/392437/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 392437,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/392437/?format=api",
"text_counter": 259,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kama huu tulionao hivi sasa, serikali zimeundwa mashinani na kuna wafanyikazi wa aina mbili; wale ambao walikuwa wanafanya kazi katika zile Serikali za Wilaya na wafanyikazi ambao hivi sasa, wataajiriwa na serikali za kaunti. Katika mtafaruku kama huu, ni lazima Serikali ikae macho kuona ya kwamba hakuna hata mfanyikazi mmoja ambaye atafutwa kwa sababu ya Serikali kugeuza njia ya kutawala nchi hii wakati wa ugatuzi. Tusiwe na mfanyikazi hata mmoja kutoka kwa Serikali za Wilaya ambaye atapoteza kazi. Litakuwa jambo la kusikitisha sana kuona ya kwamba ni wakati huu haki ya mfanyikazi inaweza kupotea. Kwa mfano, amepoteza malipo yake ya uzeeni ama malipo ya miaka ambayo ameifanyia Serikali kuu kwa sababu ya kuchukuliwa na Serikali ya kaunti. Kutakuwa na hali ya mtafaruku wakati wa kubadilisha kazi hizi na itabidi TA ikae katikati kuona ya kwamba haki imetendeka na hakuna mfanyikazi hata mmoja ambaye atapoteza haki yake ama malipo ya marupurupu yake ya uzeeni wakati ukifika wa kuacha hiyo kazi ama wakati wa ugatuzi. Bi. Spika wa Muda, ninasema hivyo kwa sababu wafanyikazi hawa wana familia zao na majukumu tofauti tofauti katika familia zao. Wako na watoto kwenye vyuo vikuu, shule za upili na zile za msingi. Wengine wamechukua mikopo ya benki ili kusuluhisha matatizo ya kifamilia ya afya na kadhalika. Na katika hii hali yote, utaona kwamba watu kama hawa, haitakuwa vyema wakiambiwa kwamba hawana kazi kwa sababu ya ugatuzi wa Serikali. Ni lazima tuelewe ya kwamba kufuatana na sheria za kimataifa za wafanyikazi, wakati kuna ugeuzi wa aina yoyote ya Serikali, mfanyikazi asipatikane na hasara ya kupoteza kazi yake. Hiyo ni sheria ambayo inatambulika na ni kwamba sisi kama Seneti, ni lazima tuone ya kwamba tumetetea kitengo hiki cha hali ya kitaifa ya wafanyikazi. Kaunti ya Kilifi ina wafanyikazi wengi sana wanaofanya kazi katika hoteli. Kuna wafanyikazi wengi ambao wanafanyakazi katika supermarkets na kulingana na Katiba ya Kenya tulioipitisha kama Wakenya, inasema kwamba, katika muda huu ambao tunageuza mwenendo wa Serikali, ni kwamba asili mia 70 ya wafanyikazi ni lazima watoke katika lile eneo la ile biashara. Hata Katiba inasema kwamba wafanyakazi wote watakaojiriwa wawe ni asilimia 70 kutoka eneo ambalo ile kampuni inafanyia kazi. Hivi majuzi jambo la kusikitisha ni kwamba katika mahoteli tukiangalia katika Kaunti ya Kilifi asilimia 70 ni kinyume cha Katiba. Utapata kwamba asilimia 30 ndio wa Giriama na asilimia 70 si wakaazi wa pale. Hili ni jambo la kusikitisha kwa sababu haliambatani na Katiba ya nchi yetu. Kwa hivyo, mimi naunga mkono nikisema kwamba hata wale wafadhili wanaoweka makampuni yao, wazingatie Katiba ya Kenya. Inafaa wajue kwamba mtu akitaka kuanza"
}