GET /api/v0.1/hansard/entries/392441/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 392441,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/392441/?format=api",
    "text_counter": 263,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "kutakuwa na njama nyingi kwamba huyu ni wangu na huyu si wangu, huyu afutwe na yule asifutwe. Ikiwa harakati zitakuwa kama hizo tunahitaji kuwa na TA ambayo itajua kwamba wafanyakazi wa kutoka serikali za wilaya lazima wapewe haki yao. Ili kuona kwamba hakuna mtu ambaye anapoteza kazi yake tunafikiria kwamba afisi ya gavana pekee yake haiwezi kufanya kazi hiyo. Kwa hivyo, inahitaji kusaidiwa ili kuona kwamba wafanyakazi wote wameondoka kutoka kwa serikali za wilaya na kuingia katika serikali za kaunti. Jambo la mwisho tunajua nchi hii ina Katiba na tunaiheshimu. Wakati kama huu tunaweza kuona wafanyakazi wakiwa kwa vyama tofauti tofauti, kwa mfano, LocalGovernment Workers Union . Ikiwa wanaweza kuhusishwa katika mipangilio hii, basi huenda pia wakachangia vilivyo kuona kwamba hakuna hata mfanyakazi mmoja ambaye haki yake imeathiriwa. Bi. Spika wa Muda, nataka kuunga mkono Hoja hii ya Sen. Elachi kuwa TA wapatiwe muda wa kukamilisha kipindi chao. Mimi sikubaliani na magavana kuwa wanaweza kuendesha shughuli za kaunti bila TA. Kwa hayo machache, ninaomba kuunga mkono Hoja hii."
}