GET /api/v0.1/hansard/entries/392770/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 392770,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/392770/?format=api",
    "text_counter": 300,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mbura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13153,
        "legal_name": "Emma Mbura Getrude",
        "slug": "emma-mbura-getrude"
    },
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda kwa nafasi hii. Kwanza ningependa kupongeza Kamati ambayo imeleta Ripoti hii ambayo imewasilishwa hapa na Sen. (Dr.) Kuti. Ni mapenzi yangu kwamba siku za usoni watafika pwani. Najua kwamba safari ya maili elfu moja huanza na hatua moja. Najua hii ni hatua ya kwanza na wataendelea kutembea ili wafike kila sehemu ya Kenya na kutuletea Ripoti ya jumla ambayo huenda itasaidia taifa hili. Bi. Spika wa Muda, pengine kwa kuongezea, ningependa kusema kwamba hawajafika eneo la pwani. Kuna maswala mengi ambayo tukijadiliana, huenda tukasaidiana. Shida ambayo tuko nayo kwa upande huu si kwa sababu ya Serikali sana bali ni kwa sababu ya madaktari wenyewe. Nikizungumzia kuhusu pwani, utapata kwamba katika district hospitals, tuseme kwamba mama amepatikana yuko na fibroids ama mzee amepatikana na prostrate cancer na watu hawa wanahitaji operation, lakini kuna uhaba wa madaktari. Utapata kwamba daktari ni mmoja na wagonjwa ambao wanahitaji operation ni zaidi ya mia moja. Kwa hivyo, watu watapewa nambari kutoka moja hadi mia moja."
}