GET /api/v0.1/hansard/entries/392776/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 392776,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/392776/?format=api",
    "text_counter": 306,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mbura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13153,
        "legal_name": "Emma Mbura Getrude",
        "slug": "emma-mbura-getrude"
    },
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda. Utapata kwamba wagonjwa wamepewa nambari kutoka moja hadi mia moja. Kwa sababu ya uhaba wa madaktari inabidi watu wengine kufariki kabla hawajafikiwa. Kwa sababu ya hili huwa inabidi watu kuwaona daktari kwenye hospitali yake ya kibinafsi. Kwa hivyo sisi ambao tuko na uwezo wa kumuona kwenye hospitali yake, tunaangaliwa kwa nambari ya mbele. Hili jambo linaumiza wananchi wengi ambao ni maskini. Kwa hivyo kuna wengi ambao wanakufa. Nimeshuhudia kisa hiki katika hospitali ya Mariakani. Bi. Spika wa Muda, tukiangalia upande wa akina mama kujifungua, ni jambo ambalo halijatiliwa maanani. Kama vile Katiba yetu imesema, kila Mkenya ana haki ya kuishi. Kwa hivyo kuna akina mama ambao wanajifungua kabla wakati kufika na tunapata kwamba hospitali zetu hazina vifaa vya kuhifadhi wale watoto. Kwa hivyo inamaanisha kwamba ikiwa hatutahadhari, watoto watakaozaliwa kabla ya miezi tisa hawataishi kwa sababu hakuna vifaa vya kuweka watoto wale ama kuwahifadhi mpaka watakapofikisha miezi yao ya kuzaliwa na kuweza kutolewa. Pia ningependa kusisitiza kwamba tunalaumu Serikali kwa sababu hawana madawa ya kutosha lakini madaktari hao ndio wanaomiliki hospitali za kibinafsi. Kwa hivyo utapata kwamba yale madawa ya Serikali ndio yanabebwa na kutumiwa katika hospitali zao za biashara. Pia wakati mwingine utaona kwamba daktari amekutibu katika hospitali yake ya kibinafsi lakini madawa unaenda kupewa katika hospitali ya Serikali. Huu ni ufisadi wa hali ya juu na ningependa Sen. (Dr.) Kuti na Kamati yake kutilia maanani maswala haya. Tumeona ya kwamba pesa inayotumwa na Serikali kuu haitoshi. Hili jambo limeleta mtafaruku ambapo madaktari wamekataa kulipwa na serikali ya kaunti; wanataka kulipwa na serikali kuu. Haya pia ni maswala ya kutilia maanani katika Kamati yenu. Pia ningependa Kamati kuangazia jambo la l odgings . Hizi ni nyumba ambazo watu wanaenda kustarehe na wanatumia mipira na mara nyingi utapata kwamba wamezitupa. Hili ni swala la afya ambalo yafaa litiliwe maanani. Baada ya starehe zao mwenye nyumba yafaa alinde wakaazi wenye eneo hilo. Mipira ile inapotupwa, watoto wetu hufikiri ni vibofu wakafurisha na ilhali wengine waliotumia wana maradhi ya ukimwi. Tumeona jambo hili kule Mombasa. Watoto wengi wameathirika kwa sababu ya mipira kutupwa ovyo. Bi. Spika wa Muda, pia ningependa kusema kwamba katika makampuni ambayo yanaendesha shughuli zao katika sehemu zetu tunapoishi kama Athi River, KenGen, hizi ni kampuni ambazo zimeleta madhara makubwa sana. Ukiangalia Athi River ambayo inatengeneza simiti, miti yote imezibwa na simiti na kumezuka maradhi mengi. Mimi nafikiri kwamba ingekuwa bora kwa makampuni kama haya kujenga hospitali ama kusaidia kuweka dawa katika hospitali zetu. Kuna kitengo kwa shirika la National Environment Management Agency (NEMA) ambacho kinasema kwa Kiingereza “polluter pay”. Haya ni maswala ambayo yafaa tuyatilie maanani. Kuna watu ambao wamekuja kufanya biashara kwenye nchi yetu na wanatuletea madhara lakini hatujatilia maanani kwamba inafaa kusaidia Serikali yetu katika kudumisha afya ya wananchi. Bi. Spika wa Muda, nikimalizia, ningependa kusema kwamba Serikali ya Kenya iliweka sheria nzuri sana ya kwamba watoto wa miaka mitano kurudi chini wapate The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}