GET /api/v0.1/hansard/entries/393527/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 393527,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/393527/?format=api",
"text_counter": 215,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": "Ninakushuru sana, Bw. Naibu Spika. Pengine utaniongezea muda wangu. Mbunge wa mashinani au Bunge la Kaunti anapata mshahara wa Kshs40,000 kwa mwezi. Pesa hizi ni za mahitaji yake yote. Wabunge wa mashinani hutembea umbali wa kilomita nyingi ili wafike katika bunge zao. Sehemu fulani wanatembea zaidi ya kilomita 200 na kila siku ni lazima wahudhurie vikao katika bunge zao. Tunajua sheria vizuri; ni lazima kulipa unapokula. Hakuna cha bure katika nchi hii. Ni aibu iliyoje kuwa mwisho wa mwezi, hawana chochote cha kupelekea familia zao. Tume ya SRC imekosa heshima kwa viongozi waliochaguliwa na wananchi kule mashinani. Tume hii hughugulikia sana mishahara na marupurupu ya wanafanyikazi wa Serikali. Wafanyikazi hawa hawakuchaguliwa na wananchi kama sisi viongozi. Ikiwa wewe ni mwakilishi wa watu katika Seneti, Bunge la Kitaifa au kiongozi katika Serikali ya ugatuzi, unafaa kuheshimiwa. Tume ya Serem hujihusisha sana na mishahara na marupurupu ya watu wake. Wao hawakusikia uchungu kutembea hapa na pale ili wachaguliwe kama sisi. Sisi tuna kazi nyingi za kuwahudumia watu wetu. Kazi yao ni kukaa ofisini na kurudi nyumbani kwao jioni. Mafuta ya gari Gari hulipwa na Serikali. Chai ya saa nne asubuhi ni ya bure, wafanyikazi wa nyumbani wanapatiwa na Serikali. Pia, wanapatiwa nyumba za bure kutoka kwa Serikali. Wao wanaishi maisha ya kifahari. Maisha yao ni ya faraja. Kwa hivyo, hawajali jinsi watumishi wa watu huko mashinani wanavyoishi. Sisi huaibika sana tunapokwenda mashinani. Tutawaeleza watu wetu nini? Ningependa mama huyu aje hapa tumuulize maswali kuhusu mishahara ya viongozi wa mashinani. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}