GET /api/v0.1/hansard/entries/393528/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 393528,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/393528/?format=api",
"text_counter": 216,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": "Naunga mkono yote yaliyosemwa na mwenzangu aliyenitangulia hapa. Sisi tunafaa kupitisha Hoja ya kutokuwa na imani na Tume ya SRC. Makomishna wa Tume hii ni watumwa. Watumwa hawana makosa lakini wale wanaowatuma ndio wenye uamuzi juu ya mishahara. Ikiwa waliweza kusuluhisha suala la mishahara ya Wabunge siku moja kwa nini wasifanye hivyo huko mashinani? Kwa nini hawaoni jambo na kulisuluhisha mara majo? Wamekuwa vipofu na hawasikii. Kwa hivyo, Bi. Serem ametumwa na Serikali ya Jubilee. Kwa nini hamtaki tuseme ukweli? Pengine kiongozi wa walio wengi hapa Seneti ambaye ametoka upande wa Serikali ya Jubilee ataleta Mswada hapa wa kusuluhisha janga hili. Hayo ni machozi ya mamba wala si kulia bali ni kufurahia mlo. Sisi si washenzi, baradhuli au wapumbavu kutokuelewa na kuona linaloendelea. Pengine kutoka juu hawataki Serikali ya Ugatuzi. Wakati mimi nikipinga katiba ilipokuwa ikitengenezwa nikisema kwamba kuna gharama, wakamfunga Sen. (Dr.) Machage jela. Majuto ni mjukuu, huja baadaye. Lipa! Kwa sababu wakati huo tulikuwa tunatengeneza sera ya mtu kwamba akistaafu awe na jina kwamba alileta Katiba. Lipa basi. Kila kitu kina gharama yake. Mnataka watu wapige magoti kuwahusudu ili mradi wapate chakula. Kipengele cha haki ya binadamu ambacho kiko ndani ya Katiba ni kwamba kila mtu ana haki ya chakula, nyumba, maji na afya. Si sheria kwamba hao wenzetu wateswe, wasononeke, walie wakati wengine wanafurahia chakula. Sasa wamegoma na mabwenyenye sasa wanatengeneza mali kwa jina la gavana. Wakisikia kwamba Seneti inataka kuunda kamati ya kufanya maendeleo, wanalia na kusononeka. Hawataki kwa sababu mbwa sasa una mfupa lakini ukitaka kuuchukua, anakukodolea macho na meno. Sisi ndio watunga sheria. Kutokana na usanii wetu tukatunga sheria na kuwapa nguvu makamishna. Sasa tunajuta. Wakati umefika kwa sisi kama viongozi tuketi na kutafakari kwa uangalifu na tuone vipengele kadhaa wa kadhaa ndani ya sheria ambavyo havistahili kamwe katika taifa letu la Kenya. Mojawapo ni kupunguza tume hizi. Kazi yao ni kufuja mali ya Serikali na hawana kazi ila kwenda kwa harusi, matanga na kadhalika kuropoka ropoka, kutukana walioteuliwa na kuwaita majina kwa hela ambazo tumewapa. Hayo hatutakubali. Muda wa wiki mbili ni wakati mwingi wa kumuita huyu Bi. Serem aje hapa. Mwenzangu Sen. Kiraitu amesema majuma mawili lakini mimi nasema waje kesho, kesho kutwa au mtondogoo. Tusingoje majuma mawili wenzetu wakiteseka kwa sababu waliambiwa na huyu Sarah Serem kwamba watafutwa kazi. Yeye amejichukulia madaraka ya wananchi na kuwaambia walioteuliwa na kuchaguliwa kwamba yeye ana uwezo wa kuwafuta kazi kwa sababu hawaendi kazini na ilhali yeye hawapi uwezo wa kwenda kazini."
}