GET /api/v0.1/hansard/entries/393542/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 393542,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/393542/?format=api",
"text_counter": 230,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, nataka kumpongeza dada yangu, Sen. Elachi, kwa kuleta Hoja hii. Kitu ambacho nataka kufafanua zaidi ni upande wa Katiba. Mimi kama mwanasheria, nahisi kuwa kuna umuhimu wa kuthibitisha sheria za Katiba. Kulingana na Kipengele cha 96, kinasema kuwa jukumu letu si kuwakilisha peke yake, bali ni kulinda na kutetea rasilmali za kaunti na serikali zake. Hiyo, kisheria, haina haja ya kufafanua zaidi. Kazi ya Seneti hapa ni kulinda na kutetea serikali za kaunti. Kwa hivyo, ni makosa kuona ya kwamba shirika linaloangalia suala la mishahara ya wafanyikazi wa Serikali halizingatii kuona ya kwamba wafanyikazi kama hao waliochaguliwa na wananchi wameweza kuishi katika hali ya kutambulika na kiheshima. Hasa nikizingatia zaidi ya kwamba waheshimiwa ambao wapo katika bunge za kaunti ni watu muhimu sana kwa sababu wao ndio wanaoshiriki zaidi, wakizingatia haki na kuwatetea wale walio huko mashinani ili kuhakikisha ya kwamba hali za maisha yao yamekuwa bora zaidi ya vile walivyo. Pia wanayo majukumu mengi kwa sababu kila wiki utaona ya kwamba mheshimiwa ambaye yuko katika bunge la kaunti ana mradi fulani anafanya. Mimi mwenyewe nimeweza kwenda nyumbani kila wiki na nimeweza kushirikiana nao upande wa kugharamia mazishi, gharama ya hospitali, karo za shule na basari. Na ukiangalia zaidi, utaona kwamba ule mshahara wanaopewa haufai hata kidogo kwa mtu kama yule kuitwa mheshimiwa. Ukiangalia mshahara wanaopewa wa Ksh79,000, ukikatwa kodi, unabaki kama Ksh50,000. Je, pesa hizi zitamsaidia mtu huyu namna gani kujikimu kimaisha na kuweza kuwasaidia wengine? Jambo hilo halitawezekana. Bw. Naibu Spika, tunamheshimu sana mama huyu kwa sababu analo jukumu kama Mwenyekiti wa Tume la kuangalia mishahara ya wafanyikazi wa Serikali. Lakini ikiwa yeye atakuwa kama yule mnyama anayeitwa mbuni, ambaye tabia yake ni kuwa akiona adui anakuja, anachimba chini na kuzika kichwa chake halafu hataki kusikia kama kuna kelele ama kuna nini maanake mwili wake unaonekana kama kichaka. Nafikiria The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}