GET /api/v0.1/hansard/entries/393543/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 393543,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/393543/?format=api",
"text_counter": 231,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "wakati wa mama huyu kujificha kama mbuni umekwisha. Kunao umuhimu wake kukaa na kufahamu ya kwamba ikiwa yeye anapata mshahara wa mamilioni, basi kunao waheshimiwa katika bunge za kaunti ambao wanapata mshahara wa Ksh79,000 kwa mwezi; na kunao umuhimu kuona ya kwamba zile pesa wanazopata zimeongezwa. Tunajua kabisa kuwa sheria za leba za wafanyikazi zinazosema ya kwamba mfanyikazi anayelipwa vizuri huwa pia anayo bidii ya kufanya kazi. Lakini mfanyakazi ambaye humlipi vizuri hana budi kukuibia wewe mwenyewe kama tajiri. Tunaanza mfumo ambao ni wa kusikitisha kwa sababu ikiwa hawa tumewapatia jukumu kama waheshimiwa katika bunge za kaunti, na mapato yao ni Ksh79,000, na pale kuna zabuni zinapeanwa na wao kama waheshimiwa wanaokaa katika ile bodi ya kugawa zabuni, ni kitu gani kitamfanya asiwe mpotovu akakubaliana na maneno anayoambiwa akapeana zabuni ili apate pesa zaidi za kujimudu? Hatutaki mambo ya ufisadi. Kwa hiyo, mimi naona ya kwamba hizi pesa wanazopata, Kshs79,000, hazina heshima hata kidogo kwa wao kuitwa “waheshimiwa.” Pesa hizi zinafaa ziongezwe ili waweze kusaidia wananchi wa huko maeneo ya chini. Ugatuzi unamaanisha kwamba mamlaka yatashuka chini na yataenda mpaka kwa mwananchi; na mwananchi atakuwa na haki ya kujua serikali yake inaendelea namna gani. Na wale ambao wanatekeleza jukumu lile na kuwaambia wananchi mambo kama yale. Hawa si wengine bali ni waheshimiwa wa bunge za kaunti. Ikiwa Serikali hii ya Jubilee inazingatia mambo ya ugatuzi, basi haina haja ya sisi kuilazimisha kuona ya kwamba wamefanya kitu kama hiki. Nashukuru sana kwa sababu Hoja kama hii imeletwa; na si lazima kuletwa na mtu ambaye anatoka katika upande wa Jubilee ama upande wa CORD. Hili ni jambo muhimu sana ambalo linahusisha taifa nzima. Kwa hiyo, mimi naona kwamba Hoja hii ni nzuri na kuna haki kusema kuwa Tume ya Sarah Serem aidha ikae chini kwa wakati mfupi na kuzingatia mambo haya, ama sivyo, serikali za mashinani zitaanguka kwa sababu hivi sasa zimekwama. Ukiangalia gavana ni mtu ambaye hivi sasa hana yule ambaye anamchunga. Ikiwa magavana hawana watu wa kuwachunga, basi baadhi yao wanaoweza kutumia mamlaka hayo vibaya. Ikiwa sisi tutatetea haki za kule mashinani kama Seneti, basi kuna umuhimu kuona ya kwamba waheshimiwa hawa wameongezewa mishahara yao. Jambo la kusikitisha ni kwamba ikiwa sisi hapa katika Seneti kazi yetu ni kulinda maslahi, rasilmali na serikali za ugatuzi, hiyo ikiwa ndio sheria ya kwanza ya Kipengele cha 96 katika Katiba, itakuwa tunafanya nini sisi kama Seneti hapa ikiwa hatuwezi kulinda kipengele hicho? Ni lazima wale waheshimiwa wa bunge za kaunti wawe kama waheshimiwa wa bunge za kaunti, na waongezwe mshahara wao na Sarah Serem katika muda mfupi unaokuja. Bw. Naibu Spika, ninaunga mkono Hoja hii."
}