GET /api/v0.1/hansard/entries/393756/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 393756,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/393756/?format=api",
"text_counter": 167,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Spika wa Muda, nakushukuru sana kwa nafasi hii ili niweze kuunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na Sen. (Prof.) Lonyangapuo, ambaye ameonyesha kuwa anajali taifa hili na wala sio tu kaunti yake anayoiwakilisha hapa. Hoja hii inahusu nchi nzima na rasilmali zetu. Bw. Spika wa Muda, nimeamua kuzungumza kwa Kiswahiil ili niweze kutafakari na kukumbuka maneno ya wimbo mmoja ambao ulikuwa unaimbwa zamani nikiwa kijana. Ulikuwa unasema kuwa ukitaka kuisaidia nchi hii, nunua mali ya Kenya. Ulikuwa unasema kuwa Bw. Kamau ananunua mali ya Kenya na kwa hivyo, anaongezea uchumi wa nchi hii nguvu sana. Wimbo huo ulikuwa unataja karibu kila kabila katika taifa letu. Bw. Spika wa Muda, tulipopata uhuru wetu, Serikali ya kwanza ya hayati Mzee Jomo Kenyatta iliweza kujimudu sana na kuanzisha viwanda mbalimbali. Tumesikia kuhusu Kicomi. Kulikuwa pia na KTM, RIVATEX, KMC, Shirika la Reli na viwanda vingine vingi. Nikiangazia Hoja hii, ningependa kusema kuwa ni aibu sana kwa taifa hili kuwa na ukosefu wa kazi ilhali watoto wetu wamesoma. Tegemeo la watoto hawa ni nchi hii. Lakini kila wakati nafasi ndogo inapotokea tunaifunga. Bw. Spika wa Muda, katika Kaunti ya Machakos ambayo ninaiwakilisha hapa kuna viwanda vingi katika mpangilio wa EPZ. Kati ya hivi viwanda, vingi vimeamuriwa kufungwa. Wakati EPZ ilianza, makampuni mengi yalienda kule na kuanza kufanya kazi, kuajiri watu na kutoa huduma. Lakini cha ajabu ni kuwa miaka 50 baada ya Uhuru wetu, tukiwa na mkonge, pamba na vitu vinavyohitajika kutengeneza nguo, nchi yetu inaweza kuendela sana. Tuna kiwanda cha Bata kinachotengeneza viatu. Nimenunua viatu vya Bata na ninaweza kuthibitisha kwamba vinadumu zaidi kuliko viatu vinavyotoka nje ya nchi hii. Pia bei yake ni nafuu. Ukinunua kiatu kwa bei ya dola 50 hapa, utakinunua kiatu kama hicho ulaya kwa dola 200. Bw. Spika wa Muda, tuko na ngozi lakini mavazi yanayovaliwa na askari wetu wa General Service Unit (GSU) na wanajeshi wetu yanatoka nje ya nchi. Kwa maoni yangu, huu ni ukora tu. Kuna watu wanaotaka kuiba pesa za Serikali. Tukinunua bidhaa kutoka kwa kampuni zilizoko nje ya nchi, tunapoteza pesa za kigeni ambazo tunahitaji. Pesa hizo zinapelekwa nje na kumlipa mtu kule India au Malasya. Pili, tukishapoteza pesa hizo na nchi kuwachwa na lawama ya kutafuta pesa za kigeni, faida inayopatikana kule haitozwi kodi hapa. Kwa hivyo, tunapoteza pesa na kodi. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}