GET /api/v0.1/hansard/entries/393758/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 393758,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/393758/?format=api",
"text_counter": 169,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bidhaa ambazo zinanunuliwa kutoka nje ni ghari muno. Kama tunanunua nje ya nchi hii shati, suruali aina ya kaki na batisi ya kufunga soksi katika kiatu cha askari jela, je, tunaweza kusimama hapa na kusema kwamba sisi ni nchi huru? Ikiwa ni lazima tuagize kutoka ng’ambo nguo za kuvaa, je tutasema nchi ni huru. Kizingizio ni kwamba, watu wanapitia mlango wa nyuma na kusema kwamba hata kwa miezi mitano hawataki tuwalipe. Wanataka tulipe baada ya miasi sita. Na hiyo miezi sita tunalipa kwa gharama ambayo watoto wetu hawatapata rasilmali yoyote. Bw. Naibu Spika, Serikali inasema kwamba inajenga vyuo vya ufundi ili kufunza watoto wetu jinsi ya kufanya kazi kama hii. Tukijenga shule hizo na watoto wetu wahitimu katika masomo yao, watapata kazi wapi? Hata wakishona zile nguo za askari jela hatutaki kununua kwao. Pesa ambazo zinabaki tunachukua na kupeleka vijijini na kujenga polytechnic ambayo haitumiki. Watoto wanakaa bila kazi na mwishowe wanakuwa wezi. Hata anakuwa seremala ilhali hawezi kuuza bidhaa zake. Juzi tumeshuhudia kasheshe na sarakasi; kizaazaa cha wasomi wakitaka kwenda China kuletea Bunge letu viti tutakavyokalia katika Bunge la Kumi. Wakati mambo yalizidi, tuliwashambulia kufa na kupona mpaka wakabadilisha nia yao. Walitoa kandarasi kwa Kiwanda cha Kenya Prisons kupitia mlango wa nyuma ili kutengeneza viti ambavyo vinatumika bungeni. Ukilinganisha vile viti na hivi tunavyokalia ambavyo vimetoka nje, ninaweza kusema kwamba hii ni takataka. Tena juzi tulisikia kwamba Parliamentary Service Commission (PSC) inataka kwenda China kutafuta viti ilhali viti viko hapa. Mikeka ambayo inafaa zaidi inashonwa kutoka mkonge. Sisi tunaletewa mikeka ya kisasa na tukitaka kuyasafisha ni lazima twendee wale waliotuuzia. Ingelikuwa tunawapa kina mama wa nchi hii nafasi ya kututengenezea mikeka tungekuwa wenyeji na wale kina mama hata wana uwezo wa kupaka zile mikeke rangi yoyote. Lakini kila msomi akitoka chuo kikuu akipewa kazi ya procurement, anakimbilia kununua mikeka ng’ambo na kupuuza yetu. Jambo hili linaudhi sana. Bw. Naibu Spika, hatufai kuisihi Serikali ibadilishe huo mwenendo na kutoa haki kwa Wakenya, nikiwa Seneta wa Machakos, ningetaka kusema kwamba Wakenya wanawaamrisha mkome ngoma na sarakasi hizi ya kununua bidhaa kama hizo kutoka ng’ambo, na wafanye mipangao kulingana na mahitaji ya Wakenya. Tunataka kutumia mali yetu, kuishi kwa haki na kutumia uwezo wetu ili watoto wetu wanaosoma wakihitimu wapate tunatumia mikeka ya mkonge na waiongezee manufaa zaidi. Hiyo ndio teknolojia ambayo tunahitaji. Tumekuwa watu wa kuwafuata wazungu. Inafaa tujitoe katika hali hiyo na tuzingatie Hoja hii ili tuhakikishe kwamba Wakenya wanaishi kwa hali inayofaa. Ninaunga mkono."
}