GET /api/v0.1/hansard/entries/393884/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 393884,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/393884/?format=api",
    "text_counter": 61,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 179,
        "legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
        "slug": "wilfred-machage"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi hii. Ningependa kuunga Hoja hii na kumpongeza mwenzangu, Sen. Karaba, kwa kuleta jambo ambalo ni la hekima, haswa kuangalia mazingira sehemu tofauti tofauti nchini, sehemu zingine za nyanda za juu na zikiwa na milima mingi. Jambo hili linaweza kutekelezeka kwa kuleta Hoja ya kuomba Serikali Kuu ili iweke halmashauri ya kuangalia jambo la kutengeneza gari za waya. Ningependa kuunga mkono na kusema kwamba hili jambo laweza pia kufikiriwa na Serikali ya Ugatuzi. Hivi leo mkiangalia kwa magazeti na vyombo vya habari, serikali za ugatuzi zimeshindwa kutumia hela. Hela zimefurika kwa benki, sijui ni kwa sababu hawana mipango kamili lakini mambo kama hayo pia yangefanywa kwa daraja hilo ili kutekeleza wazo letu nchini na kuendeleza mambo yetu ya uchumi kama utalii. Hapa, tuna lengo la kuwa na watalii karibu million tatu kila mwaka. Hilo ni jambo la aibu kwa sababu nchi hii ina uwezo wa kuwa na watalii zaidi ya millioni kumi kila mwaka, haswa ukiangalia sehemu nyingi nchini: Upande wa magharibi kuna Ziwa Victoria ambalo halitumiki kabisa, kwenye nyanda za juu, kuna Mlima Kenya na Aberdare, upande wa kusini kuna Taita Taveta ambapo tunaweza kutumia vifaa hivyo kusudi watalii wanapotembea huko wasigutushe wanyama ambao wako chini kuliko kutumia magari au ndege aina ya helikopta zenye kelele nyingi. Kwa hivyo, hili sio jambo la kutafakari kwa siku nyingi. Hili ni jambo ambalo linaweza kutekelezeka. Yafaa tuwe na mipango kamili kwa sababu tuko na uwezo, nia na lengo. Kwa hivyo, hatuwezi kushindwa. Sina mengi ya ziada ila kuunga mkono."
}