GET /api/v0.1/hansard/entries/393891/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 393891,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/393891/?format=api",
"text_counter": 68,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mbura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13153,
"legal_name": "Emma Mbura Getrude",
"slug": "emma-mbura-getrude"
},
"content": "Asante, Bw. Naibu Spika, kwa nafasi hii. Ningependa kumpongeza Seneta Karaba kwa kuleta Hoja hii nzuri sana ambayo inalenga kwetu pwani. Tukiangalia uchumi wetu wa Kenya unachangiwa na utalii. Tukiangalia kama kwetu pwani, kuna mahali pengi sana ambapo shughuli za utalii zinaweza kunawiri, lakini zimefifia kwa sababu ya barabara. Usafiri umeleta changamoto kwa watalii kuweza kufikia maeneo fulani. Kwa mfano, Mekatilili ambaye alikuwa mpiganiaji Uhuru wa nchi yetu ya Kenya, ni mama aliyejulikana sana ulimwengu mzima na kila mtalii anayetembelea nchi ya Kenya hutamani kujua pahali yule mama alikozikwa, lakini imekuwa ni vigumu sana kwa watalii kufika mahali pale. Kama Hoja hii ingeweza kutekelezwa na tukapata hizi"
}