GET /api/v0.1/hansard/entries/393893/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 393893,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/393893/?format=api",
"text_counter": 70,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mbura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13153,
"legal_name": "Emma Mbura Getrude",
"slug": "emma-mbura-getrude"
},
"content": ", itakuwa ni rahisi watalii kuweza kufika mahali alikozikwa kule Bangale, Malindi. Shughuli kubwa sana za utalii hapa kwetu Kenya, tunaona zimelenga hoteli zilizoko kwenye ufuo wa bahari. Na utaona kwamba kuna shida kutoka Kiwanja cha ndege cha Mombasa hadi mahotelini ilhali ni sehemu ambayo ingechukua hata dakika kumi, lakini siku hizi tunachukua hata masaa sita. Wakati mwingine magari yanakwama ukifika mahali panapoitwa Changamwe ama Kipevu. Kuna msongamano wa magari na wakati mwingine magari yanakwama pale kwa masaa 24; hayaendi na hayarudi, kwa sababu njia inayotoka kwenye uwanja wa ndege kuelekea Nairobi ama kuingia Mombasa, ama kuenda Jomvu, kuna msongamano mkubwa wa magari. Lakini tukiwa na cable cars, tungerahisisha utalii wetu. Hasa wakati wa Krismasi watalii wanapokuja hapa nchini, huwa wanakwama kwenye uwanja wa ndege. Hata wakati mwingine Krismasi inaishia kwa usafiri. Bw. Naibu Spika, kungekuwa na cable cars, zingesaidia kwenye Kivuko cha Likoni. Huwa kuna msongamano kwenye Kivuko cha Likoni kwa sababu kuna uhaba wa feri. Lakini leo hii tungekuwa na cable cars, zitatusaidia katika kuwavusha watalii wetu kufikia maeneo ya utalii ambayo yako upande wa Kwale, kuingia katika hoteli zetu za kitalii upande wa Likoni. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}