GET /api/v0.1/hansard/entries/393898/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 393898,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/393898/?format=api",
    "text_counter": 75,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Bule",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1029,
        "legal_name": "Ali Abdi Bule",
        "slug": "ali-abdi-bule"
    },
    "content": "Nashukuru, Bw. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Pia ninamshukuru Sen. Karaba kwa kuleta Hoja hii kwa wakati ufaao. Hii Hoja ni ya muhimu na itaweza kupeleka uchumi wa nchi ya Kenya mbele. Hii ni hatua ya kisasa na yakupendeza. Ninaunga mkono Hoja hii kwa kusema kwamba Kenya inahitaji hizi cablecars kwa sababu kuna milima mingi sana hapa nchini. Pia kuna mito mahali pengi. Mimi ninatoka Tana River na kuna sehemu ambako hata mimi hushindwa kufika. Tukipata magari haya, yatatusaidia kuweza kufika sehemu mbali mbali ambazo hatuwezi kufika kwa wakati huu. Magari haya ya stima yataweza kutumika katika mahali pengi nchini. Na ninafikiri kwa sasa, katika Afrika nzima, Kenya ni nchi ambayo imenawiri na inahitaji kuwa na vifaa kama hivi. Magari haya yatatuwezesha kukwea milima na kuvuka mito mbali mbali bila shida yoyote. Juzi, nilikuwa na mkutano katika kaunti yangu, na tulishindwa kuvuka mahali fulani kwa sababu gari letu halingeweza kupita mahali hapo. Ilitubidi tutembee kwa kilomita kumi. Gari kama hili litawezesha watu kufika mahali hapo na kuwawezesha watalii kutembelea sehemu nyingi na itaweza kuongeza hazina ya nchi. Ninaunga Hoja hii mkono kwa dhati na ninawasihi wenzangu waiunge mkono ili tuipitishe kwa pamoja. Asante."
}