GET /api/v0.1/hansard/entries/394674/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 394674,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/394674/?format=api",
"text_counter": 64,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": "Nashukuru, Bwana Naibu Spika. Naunga mkono Hoja iliyoletwa na mwenzangu, Sen. Daniel Karaba. Anaiomba Seneti hii ifikirie na kutafakari kuunda njia za ziada katika barabara za jiji letu la Nairobi. Wahenga walisema; “kwa sababu ya kukosa mikono, ng’ombe alijikunia ulimi.” Tunajipata katika hali hiyo tunapokuwa na shida ama majonzi tukitaka kufika katika kituo cha usaidizi hapa jijini. Shida hii haimo hapa tu bali katika miji yote nchini. Jiji la Nairobi lilijengwa kuanzia 1901 wakati wa ujenzi wa reli. Wakati wa ujenzi wa hoteli ya Norfolk, ilitabiriwa kwamba kungekuwa na magari 300 ndani ya jiji hili. Kwa hivyo, jiji lilijengwa kwa menajili ya magari 300. Barabara zake zilijengwa hivyo. Tangu hapo, hakuna mtu ambaye ameshawahi kufikiria kuhusu kukuwa kwa jiji hili na hitaji ya kutengeneza njia za ziada. Sasa hivi, imedhihirika hasa wakati wa mikasa kwamba hatuna nafasi ya kuokoa maisha ya binadamu na mali. Lakini, tunapofikiria hivi, lazima tujue kwamba makosa yaliyotekelezwa wakati huo pia yamewaleta wawekaji rasilimali na kuwafanya wajenge manyumba makubwa na viwanda vikubwa katika nafasi ambayo ingetumika kupanua barabara zetu kwa ajili ya jambo kama hili. Hili silo jambo ambalo tulidhani lingekuwa la dharura lakini lazima liwekwe kwa mipango ya Serikali. Jambo hili linahitajika kwa njia kadhaa lakini sio zote zile zimewekwa mbele yetu. Bwana Karaba amesema kwamba njia ambazo zinaelekea kwenye zahanati kubwa kama vile Aga Khan, Kenyatta na zinginezo zitiliwe maanani ili zipanuliwe. Zinafaa kuwekewa njia maalum za ziada hasa wakati huu ambapo Serikali imejikaza kisabuni katika ujenzi wa barabara ambazo ni nzuri. Kama jambo hili limewapita basi wanafaa kulitia maanani. Nimeona katika sehemu zingine wameweka njia nyembamba za kutumika na watu wanaotembea na baisikeli. Lakini, tunataka kuwa na njia tunazoweza kutumia katika siku za shida. Aliyelipanga jiji hili alikuwa na mawazo ya mbele. Miji mingi sasa imewanyima watu kutoka kutembelea juu ya barabara za kawaida. Wamelima barabara za chini kwa chini, kuanzisha njia za reli na kadhalika. Nafikiri kuna haraka ya kulipanga jiji la Nairobi upya. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}