GET /api/v0.1/hansard/entries/394675/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 394675,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/394675/?format=api",
"text_counter": 65,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 179,
"legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
"slug": "wilfred-machage"
},
"content": "Nashukuru Serikali iliyopita kwa sababu aliyekuwa Rais Mzee Kibaki aliiteuwa Wizara ya Maendeleo ya Jiji la Nairobi. Sijui kama mawazo hayo yamefunikwa na Serikali ya sasa. Kama yamefunikwa na Serikali ya sasa, basi yanafaa kufunuliwa. Hayo yalikuwa mawazo mazuri. Jiji hili na miji mingine kama vile Kajiado, Machakos na nyingine inafaa kufanyiwa mipango mipya ya ujenzi. Nafasi inafaa kuwepo ya kujenga barabara ambazo zinaweza kutimiza maendeleo ambayo nchi hii imefikia. Nchi kama vile Amerika na zingine zimeshafanya hivyo. Twahitaji uchumi wa kutosha lakini Mungu si adhumani. Ametuangazia nafasi ya kupata mafuta, makaa na sasa hivi tunapata hata dhahabu Migori. Uchumi ambao utapatikana katika mambo hayo haufai kutumika vibaya. Unafaa kutumika kwa mipango mizuri kwa siku za usoni. Sina budi wala kuunga mkono Hoja hii."
}