GET /api/v0.1/hansard/entries/394681/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 394681,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/394681/?format=api",
    "text_counter": 71,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chelule",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13126,
        "legal_name": "Liza Chelule",
        "slug": "liza-chelule"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, sisi sote tunaelewa kwamba msongamano wa magari katika Jiji la Nairobi unaleta shida, sio tu wakati wa hatari bali pia katika uchumi wa nchi. Naunga mkono Hoja hii ingawa najua kuwa kuna shida ya nafasi. Mara nyingi tunapoendesha magari yetu katika barabara za Nairobi, tukisikia milio ya magari ambayo yanabeba wagonjwa au yale ya kuzima moto, inakuwa ni changamoto sana kwa magari hayo kupata nafasi ya kupitia. Hali hii inasababisha nyumba kuchomeka au wagonjwa kufa barabarani."
}