GET /api/v0.1/hansard/entries/394699/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 394699,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/394699/?format=api",
    "text_counter": 89,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mbura",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13153,
        "legal_name": "Emma Mbura Getrude",
        "slug": "emma-mbura-getrude"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika, kama mpaka leo container zetu za mizigo zingekuwa zinapelekwa kwa gari la moshi, nafikiri kuwa msongamano wa magari ungekuwa umeisha katika barabara zetu. Wanasiasa ndio walisababisha kuondolewa kwa mizigo katika magari ya moshi na kuanzisha biashara zao za kusafirisha mizigo kwa barabara. Usafiri wa reli ulififia na biashara zao zinaendelea barabarani hadi wakati huu. Watakapokubali kutii sheria za nchi hii na kuunga mkono uvumbuzi wa barabara za reli na mizigo yote kusafirishwa kwa magari ya moshi, huenda tukapunguza msongamano huu ambao tunaongea juu yake hapa."
}