GET /api/v0.1/hansard/entries/394700/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 394700,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/394700/?format=api",
"text_counter": 90,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mbura",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13153,
"legal_name": "Emma Mbura Getrude",
"slug": "emma-mbura-getrude"
},
"content": "Bw. Naibu Spika, ningependa pia kusisitiza hapa kwamba hizi ambulances ambazo tunazizungumzia zina hatari yake. Kuna ambulances zingine ambazo hazibebi wagonjwa. Kwa mfano, kwetu Mombasa tulikuja kugundua ya kwamba magari mengi yenye ving’ora vya kuashiria kuwa wagonjwa wanakimbizwa hospitalini huwa yamebeba madawa ya kulevya. Kwa hivyo, wakati tutakapopanua barabara hizi ili kutenga barabara za ambulance na fire brigade, Serikali inafaa kuwa macho, kwa sababu nyingi huwa hazibebi wagonjwa bali ni kusafirisha silaha na mihadarati. Kwa hivyo, pia kuna hatari yake. Tunaweza kupanua barabara kisha tukawapanulia majemedari wasioshiba, ambao wanatuharibia nchi yetu."
}