GET /api/v0.1/hansard/entries/396677/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 396677,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/396677/?format=api",
"text_counter": 125,
"type": "speech",
"speaker_name": "October 1, 2013 SENATE DEBATES 17 Sen. Hassan",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Naibu Spika, nasimama kuunga mkono Hoja hii, kwamba majukumu ya taasisi ya KeRRA yapelekwe haraka katika mamlaka ya serikali za kaunti. Bw. Naibu Spika, namshukuru sana ndugu yetu ambaye ni Seneta wa Kajiado, Bw. Peter Mositet, kwa kuleta Hoja hii. Hii ni kwa sababu tunajua kwamba kama Seneti tunajukumu la kuhakikisha kwamba tumelinda maslahi ya kaunti zetu na kuhakikisha kuwa Serikali yetu inawajibika kikatiba. Bw. Naibu Spika, kuna majukumu mengi sana ambayo serikali zetu za kaunti lazima zitekeleze. Mojawapo ya mambo ambayo yamedhoofika sana katika taifa la Kenya ni maswala ya barabara. Hivi sasa tumepata fursa ya kuhakikisha kwamba barabara zitaweza kuhudumiwa kupitia kwa mamlaka ya serikali za kaunti. Kupitia sera ya ugatuzi, tunajua kwamba tumeleta serikali karibu kwa sababu Waswahili husema: “Kiatu unachokivaa ndicho unakijua pale kina machungu yake.” Kwa hivyo, serikali zetu za kaunti zinaweza kuhakikisha kwamba zimetekeleza majukumu yao kwa kukarabati barabara zetu ndogo ndogo. Pale ambapo hakuna barabara, serikali hizi zinaweza kupendekeza ili barabara hizo zijengwe, ili tuweze kuleta hali inayofaa ya mawasiliano katika kaunti. Hii itahakikisha kuwa tunaendeleza uchumi na usafiri katika kaunti zetu. Bw. Naibu Spika, mnajua maana ya neno “kera” katika Kiswahili. Kukera mtu ni kumsumbua mtu. Ukisema: “Huyu mtu ananikera,” inamaanisha kuwa yule mtu anakusumbua au anakudungadunga.” Kwa hivyo, tunataka hii taasisi ya KeRRA isikere kaunti zetu. Warudishe majukumu ya kaunti zetu katika mamlaka ya kaunti zetu. Lile la muhimu ni kuhakikisha kwamba Serikali ya kitaifa imetii matakwa ama amri za kikatiba. Bw. Naibu Spika, wengi wamezungumza hapo awali kwamba lile swala nyeti katika maswala ya ugatuzi ni kuhakikisha kwamba tumeondoa ule ubaguzi wa kimaendeleo ambao umekuweko katika Kenya hii na wengine wetu kukataa kwamba ubaguzi kama huu umekuwepo; labda ni kwa sababu walikuwa katika upande wa kupata. Wengine wetu tumeamini, ijapokuwa tunatoka katika Kaunti ya Mombasa, kuwa tumebaguliwa kimaendeleo kwa muda mrefu. Kwa hivyo, hakuna mtu katika Kenya hii ambaye haamini kwamba kumekuwa na ubaguzi wa kimaendeleo. Kwa hivyo, tukiendelea kuangalia ni barabara zipi zitapewa kipaumbele kwa njia ya kukarabatiwa, basi tunaweza kulegeza kamba katika maswala ya kuhakikisha kwamba tumetekeleza ahadi ya ugatuzi. Bw. Naibu Spika, mara nyingi sana ni lazima pia tuchunguze--- Ningewataka wale ambao wako katika Kamati tofauti tofauti za Bunge wajaribu kuelewa ni kwa nini watu wamekwamia mamlaka haya. Niliwasikia baadhi ya wakuu katika Serikali ya Kaunti ya Mombasa wakisema kwamba sababu moja ya watu kukwama na majukumu haya ni kwa ajili kandarasi zimetolewa. Tungependa Kamati za Seneti hii ziweze kufuatilia ni kwa nini watu hawataki majukumu haya ya KeRRA kurudishwa katika kaunti zetu. Inamaanisha kwamba kuna mtu ambaye labda amekalia jambo fulani na huenda zile shutuma zilizoko ni za ukweli. Mara nyingi sana tunajenga barabara ndogo ndogo kuliko kubwa kubwa. Kwa hivyo, kandarasi zaidi ziko hapo. Hii ndio maana tunataka kuzithibiti. Kama yale malalamishi kwamba baadhi ya kandarasi zimetolewa na ndio maana watu wengine hawataki kuyatoa majukumu, basi kuna Kamati tofauti tofauti za Seneti ambazo zitachunguza mambo hayo. Kuna Kamati za mawasiliano, maswala ya fedha na zingine nyingi. Katika siku zinazokuja, baadhi ya Kamati zetu za Seneti zitakuwa zinatembelea The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}