GET /api/v0.1/hansard/entries/396679/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 396679,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/396679/?format=api",
"text_counter": 127,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kaunti, kwenda kuangalia majukumu yale ambayo yalipelekwa kule. Wale Maseneta watakaotekeleza majukumu haya wanataka kuangalia ni nini ambacho ni kizuizi kwa Serikali yetu kukabidhi majukumu ya barabara hizi za KeRRA katika mamlaka ya serikali zetu za kaunti. Bw. Naibu Spika, tukiendelea kukwamia majukumu ambayo serikali za kaunti zimepewa kikatiba, tutaendelea na sera ile ile ambayo katika fikira zetu kuna Serikali kuu na serikali za wilaya. Serikali za kaunti sio serikali za wilaya. Nilimsikia mwenzetu mmoja pale akisema: “Kama mnaogopa kuwapatia pesa kwa sababu zitaporwa, kwa nini mmewapatia pesa zingine?” Kuna watu wanaosema kuwa tukifanya ugatuzi tutakuwa tunapeleka ufisadi mashinani. Wengine wanasema kwamba hao watu sio waaminifu na kwa hivyo, wanafaa kutuletea akaunti za pesa zao. Basi kama hatuwaamini, mbona tunawapa pesa zile zingine? Tunawapa mabilioni kisha tunaogopa kuwapa Kshs200 milioni. Hizi ni fikira ambazo Waswahili wanaziita za kiabunuasi; jambo ambalo haliingii akilini. Wewe unasema kuwa huyu ni mfisadi na atapora rasilmali na huku unampa na kuogopa kumpa kile kingine kidogo. Kwa hivyo, kama sisi tuliazimia kwamba tunataka ugatuzi, tuko tayari kupambana na ufisadi. Wewe tekeleza ugatuzi na yule atakayekuwa mfisadi, sisi tutapambana naye kama taifa la Kenya. Kwa hivyo, msijaribu kutia duku duku katika nyoyo za Wakenya kwamba tukileta ugatuzi kikamilifu, huenda kukawa na ufisadi mwingi. Sisi tumewachagua watu hao na kila mmoja hapa alipigiwa kura kama Seneta. Uko na jukumu la kuhakikisha kwamba rasilmali za kaunti zimetumika kiadilifu. Kila mtu hapa amemchagua gavana wake kwa imani yake, akijua ni kwa nini. Kwa hivyo, ni lazima turegeshe yale majukumu pale yanapostahili. Bw. Naibu Spika, nataka kumshukuru ndugu yangu, Sen. Mositet na wengine ambao wametoka katika kaunti ambako barabara zilizoko zilijengwa kitambo sana. Kuna barabara nyingine ambazo hazijapanuliwa tangu wakoloni waondoke. Mkienda Mombasa, mnasema kuwa kuna dhiki kutoka airport mpaka Mombasa Town. Ni kwa sababu hakujajengwa inchi moja ya barabara baada ya wakoloni kuondoka. Barabara zingine zimewekwa viraka kwa njia ya ukarabati. Wengine kama ndugu zetu wa Lamu hawana barabara kabisa. Huenda wale ambao wamepata rasilmali sasa, kama Turkana, watanufaika kidogo. Hatuna mengine isipokuwa kujenga viwanja vya ndege vya kimataifa. Huenda hivyo viwanja pia vikaleta wafisadi wapya kwa ndege. Kwa hivyo, ni lazima tuhakikishe kwamba tumeweka zile stakabadhi ili watu wapewe majukumu yao. Ndugu zetu wengi hapa wameumia na tunajua tukipata fursa na rasilmali hii, huenda tutapata afueni. Mwisho, inafaa magavana hawa wakiondoka baada ya miaka mitano wawaonyeshe wananchi wamefanya nini. Hata sisi Maseneta inafaa tuonyeshe tumefanya nini, mbali na kuleta Hoja baada ya nyingine. Watu hutaka kuona matokeo. Ukienda Mombasa, kila mtu anauliza ni nini alilolofanya la kuleta faida kwa wananchi bali siyo yale aliyosema katika Seneti. Ukiulizwa na watu wa Migori umefanya nini, haina maana kuwaambia kwamba umechangia kila Hoja kwani mkono mtupu haulambwi. Watu wanataka kuona barabara ikijengwa. Wananchi katika kaunti wanataka kuona maendeleo. Hatufai kutegemea Serikali kuu au Rais kwa kila jambo. Na hatutajali nani ndiye Rais au Naibu wa Rais wetu kwa sababu kutakuwa na mipangilio ya kufanya kazi. Na hii ndio ilikuwa nia ya hii Katiba. Ushrikiano wa kisiasa utakuja lakini kwa mapenzi na kwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}