GET /api/v0.1/hansard/entries/396737/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 396737,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/396737/?format=api",
"text_counter": 185,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kisasa",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13124,
"legal_name": "Mshenga Mvita Kisasa",
"slug": "mshenga-mvita-kisasa"
},
"content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda. Nanafikiri kila eneo la watu kuna msemo wao. Huko pwani tunasema kwamba, “penye wazee hapaharibiki jambo”. Kwanza, ningependa kumpongeza Sen. (Prof.) Lonyangapuo kwa Hoja hii. Mimi mwenyewe nilikuwa ninapanga kuileta Hoja hii hapa kwenye Bunge la Seneti. Kwa hivyo, ni kama ameniibia Hoja hii. Mimi nina heshima kubwa sana kwa wazee wetu. Wazee na akina mama wote wana majukumu makubwa sana kule nyumbani. Kuhusu usalama, ni lazima tuzingatie kuwa wakati huu tuna ugatuzi. Ugatuzi maanake ni nyumbani ama mashinani. Ukiangalia kule mashinani, polisi mmoja hawezi kumchunga raia mmoja. Kwa hivyo, hatuna polisi wa kutosha kuleta usalama, isipokuwa kama tutaongeza wale wazee wa mtaa ama wale watu walioko kwenye vijiji ili tusaidiane na polisi kudumisha amani na usalama. Bw. Spika wa Muda, ninataka kuzungumza machache kuhusu suala la Mombasa Republican Council (MRC). Vijana wote ambao wameungana na kikundi hiki, na wale ambao wanafanya mambo ambayo hayahusiani na maadilifu kwenye jamii, tunawajua, kwa sababu ni watoto wetu na ndugu zetu. Kwa hivyo, tuwaonyeshe hao wazee kwamba tunawapenda na wakifanya shughuli fulani watapewa zawadi kidogo, kwa mfano, Kshs2,000 ambazo ni pesa nyingi sana kule mashinani. Ni wangapi kati yetu wanapeana Kshs2, 000 kila mwezi? Hawa wazee wakipewa Kshs2,000, hiyo itakuwa imewatosha na tutakuwa na usalama majumbani kwetu. Hata wale wanakula unga na kuuza madawa ya kulevya tunawajua kwa sababu ni watoto wetu na tuanishi nao. Pia tukiangalia hao wazee kwa kuwaheshimu na kuwapatia zile nyadhifa, masuala haya yote ya ukosefu wa usalama yatarudi chini. Upande mwingine, tumekuwa tukisema kwamba yetu ni Serikali ya digital . Tutawafanyaje hao wazee? Je, tuwaue? Kwa hivyo, tukiwapatia nyadhifa katika mitaa, tutakuwa tumewatia katika hii Serikali yetu ya digital . Kama kule kwetu Kilifi, imebidi wauwawe kwa sababu wanakula chakula ambacho kingekuwa ni cha watoto wao. Mimi mweneyewe nilipatikana na mtihani kwa sababu mjomba wangu aliuawa kwa sababu alikuwa ameficha Title deed au cheti cha kumiliki shamba. Kwa hivyo, inafaa tuwalete hao wazee pamoja. Utaona kwamba wakati wa uchaguzi huwa tunawavuta hawa wazee karibu sana na sisi lakini tukishapata vyeo, tunawasahau. Hatuwezi kufanya kazi bila hawa wazee wa mitaa. Ni lazima Sen. (Prof.) Lonyangapuo aliwatafuta wakati wa uchaguzi na wakamsaidi sana. Ndio sababu nilisema kwamba, ni kama ambaye ameniibia Hoja hii kwa sababu wakati wa kampeni yangu, nilitumia hawa wazee sana na ndio niko mahali hapa. Nilihakikisha kwamba hao wazee walinisaidi katika kila jambo. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}