GET /api/v0.1/hansard/entries/396739/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 396739,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/396739/?format=api",
    "text_counter": 187,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika wa Muda, hii ni Hoja ambayo imechelewa sana. Hata marehemu baba yangu pia angepata kibarua kama hiki kwa sababu Kshs2,000 ni pesa nyingi sana kule mashinani. Kwa hivyo, tukifanya hivyo, tutakuwa tumeleta amani na heshima kubwa kwa hao wazee. Nimeuliza awali ni nani humpa mzazi wake Kshs2,000 kila mwisho wa mwezi. Mimi wangu alienda mbele ya haki, na Mungu amrehemu. Lakini ninasema itakuwa ni zawadi kubwa sana kwa hawa wazee na sisi wenyewe katika ugatuzi kwa sababu kila jambo litakuwa rahisi sana. Anayekuja pale nyumbani tutakuwa tunamjua na kule anakotoka. Bw. Spika wa Muda, katika nchi ya Tanzania, kazi inayofanywa na polisi wetu hapa nchini, huwafanywa na wazee wa mtaa ambao wanajulikana kama Sungu Sungu . Hao wote wanachangia katika jamii yote. Kwa hivyo, tusiseme tumeenda digital na tukasahau kwamba tuna majukumu ambayo yanaweza kufanywa vizuri na hawa wazee. Inafaa sisi kujali masilahi ya wazee hao, badala ya kuwaacha kule mashinani kwa hali ya umasikini sana. Kwa hayo machache, ninaunga mkono Hoja hii."
}