GET /api/v0.1/hansard/entries/397782/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 397782,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/397782/?format=api",
"text_counter": 65,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Juma Boy Juma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 758,
"legal_name": "Boy Juma Boy",
"slug": "boy-juma-boy"
},
"content": "Bi. Spika wa Muda, namshukuru kwa sababu nilifikiri haelewi kumbe anaelewa. Hivyo alivyo elewa ndio ilikuwa nia yangu na wala si nia yangu kupotosha wananchi. Kuna Serikali ya Kitaifa na serikali ya ugatuzi. Kulingana na hali hii, nia na madhumuni ya hoja hii ni kuhakikisha ya kwamba nchi nzima, huu utandawazi ambao ni mwelekeo wa miaka hii, unaendelea. Kwa hivyo, namsifu aliyeleta Hoja hii. Yeye ni mwenyekiti wa kamati yetu. Naona kwamba yeye yuko na maono ya mbele. Nawaomba maseneta wote kuunga mkono Hoja hii kwa sababu inaeleza kinagaubaga nia na madhumuni yake. Pia ameeleza wazi wazi sababu za kuunga mkono Hoja hii na ifuatiliwe kikamilifu. Serikali ya Kitaifa yafaa ihakikishe kuwa jambo hili linakamilika kama ipasavvyo. Bi. Spika wa Muda, kwa hayo machache, naunga mkono. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}