GET /api/v0.1/hansard/entries/398241/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 398241,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/398241/?format=api",
    "text_counter": 376,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Shimbwa",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1345,
        "legal_name": "Omar Mwinyi Shimbwa",
        "slug": "omar-mwinyi-shimbwa"
    },
    "content": "Bi. Naibu Spika wa Muda, ningependa kulijulisha Bunge kwamba si vizuri kuwaruhusu Wabunge kuvunja nyoyo za maafisa wa usalama. Hapa tunaonekana na Wakenya kote nchini. Haifai mtu kusimama hapa na kusema kwamba maafisa wa usalama ni waoga na walishindwa kuingia kwenye jengo la biashara la Westgate, tukijua kwamba maafisa kutoka Reece Company wa kitengo cha GSU, ambao pia ni maafisa wa polisi, waliingia kwenye jengo hilo; na pia tukifahamu kwamba kuna maafisa wa polisi ambao walipoteza maisha yao kwenye operesheni hiyo. Sisi pia tunalindwa na maafisa wa polisi. Ningependa mtu akizungumzia suala hilo umukemee mara moja ili arekebishe matamshi yake."
}