GET /api/v0.1/hansard/entries/398786/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 398786,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/398786/?format=api",
"text_counter": 62,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Njoroge",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13158,
"legal_name": "Ben Njoroge",
"slug": "ben-njoroge"
},
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii, niunge mkono Hoja hii. Kwanza, nimeamua kuzungumza katika lugha ya Kiswahili ili ujumbe wangu uwafikie watu kule mashinani. Hawa ndio watu ambao hujishughulisha zaidi na kuhifadhi maji. Jambo la kwanza ambalo ningetaka kusema kuhusiana na mambo ya kuhifadhi maji ni kwamba maji yanayopotea kunaponyesha ni mengi sana. Maji haya yangewasaidia wakulima kupata mavuno kwa njia inayofaa. Itakumbukwa vizuri kwamba thuluthi tatu ya mchanga tulio nao katika nchi yetu umekuwa na kile tunachoita kwa lugha ya Kiingereza ‘hard pan’ ama meza ya maji. Mara nyingi, maji huweza kupotea kwa sababu ile meza ya maji iko juu sana karibu na mchanga kwa sababu mara nyingi urefu kwenda chini ni kama futi moja. Wakati mwingi huwa tunaachwa bila maji kwa sababu mchanga wenyewe hukosa kuhifadhi yale maji. Tumeona mara nyingi wakati kuna trakta ambayo iko na jembe lake iliyotengezwa mahasusi kubomoa ule udongo ndio maji yaweze kuingia chini ya mchanga ndio yahifadhike. Lakini wakati mwingine kukishapandwa mimea, inakuwa vigumu sana kwa yale maji kuhifadhika kwa muda mrefu. Kwa hivyo, tujaribu kuiga vile kulivyofanywa kule California katika miaka ya mwisho wa 1960s, ambapo waliweza kutengeneza dawa ambayo ingeweza kusaidia kubomoa ule udongo ili uweze kuhifadhi maji ili ile mimea iweze kutumia yale maji kwa muda mrefu. Yale maji huwa yanarudi kutumika wakati wa kiangazi na inafanya mimea kuwa mizuri ama inakua maridadi sana kulingana na soko. Bw. Spika, nikiunga Hoja hii mkono, ni vizuri pia kusema kwamba wahusika wanaokuza mimea yetu pia wafikirie vile wanaweza kutumia hiyo dawa ambayo inatumika kule California ili udongo wetu pia uweze kuhifadhi maji kule chini kwa muda mrefu. Kwa kufanya hivi, maji haya yataweza kutumika na mimea hata wakati wa kiangazi. Wakati mwingi tunapoona mimea yetu ikikosa kuwa na ile afya nzuri; na hata wakati mwingine unakuta uzito wa zao kama la kahawa unapungua sana, ni kwa sababu wakati wa kiangazi, mimea inakosa maji ya kutosha. Kwa hivyo, inapunguza ule uzito na pia hiyo inapunguza afya yake kwa njia kubwa sana. Kwa hivyo, ili mazao yetu yawe mazuri, ni vizuri tuhifadhi hayo maji ndio wakulima waweze kuwa na ukulima bora pia wakati wa kiangazi. Bw. Spika, kwa haya machache, naomba kuunga mkono Hoja hii."
}