GET /api/v0.1/hansard/entries/398826/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 398826,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/398826/?format=api",
    "text_counter": 102,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Machage",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 179,
        "legal_name": "Wilfred Gisuka Machage",
        "slug": "wilfred-machage"
    },
    "content": "Bi. Spika wa Muda, maji ni uhai. Katika mwili wa binadamu karibu asilimia 80 ni maji. Unahitaji kunywa maji yasiyopungua glasi nane kila siku, ama sivyo hutaishi. Sio sisi tu lakini kwa viumbe vyote ulimwenguni vikiwemo wanyama, miti na kadhalika. Kwa hivyo, ombi la Mama Kittony kupitia Hoja hii ni kwamba Serikali iwe na mpango kamili wa uhifadhi wa maji kwa kila jamii, kwa sehemu zote 47 za ugatuzi hapa Kenya. Bi. Spika wa Muda, hili swala limekuja wakati mzuri. Nafikiri ni Hoja ya maana zaidi kuliko Hoja zote ambazo tumeshaongea katika Seneti hii. Hivyo basi, ni lazima tutafakari na kufikiria kwa undani kabisa, tukitoa mapendekezo yetu kwa wale ambao wamepewa uwezo na kuwatumia ili kuendeleza jambo hili la uhifadhi wa maji. Sasa hivi, tunajua kwamba Jangwa la Sahara linasonga kusini kwa kiwango cha kilomita 45 kila mwaka. Hatujui itachukua muda gani - lakini hili linaweza kuthibitishwa kwa hesabu - kutufikia sisi na Kenya nzima kuwa jangwa, hasa vile kwa sababu tumeanza kuyatoboa maji ardhini na kuyafyonza. Hii ni sababu zaidi ya jangwa kuenea. Huku Kenya, nafikiri kuwa saa zingine Mungu hustaajabu. Mvua ikinyesha na kuwe na gharika, Wakenya huanza kulia. Waislamu kwa Wakristo huanza kusali wakisema: “Oh Mungu, mvua imekuja zaidi. Tuondolee janga hili. Twakushukuru.” Punde si punde, mvua inakatika. Baada ya mwezi mmoja au miwili, tunaanza tena kulia The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}