GET /api/v0.1/hansard/entries/398828/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 398828,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/398828/?format=api",
    "text_counter": 104,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "na kusema: “Oh Mungu, jua limekuwa kali, kumekauka kila mahali na mifugo wamekosa maji. Tuletee mvua.” Nafikiri Mungu saa zingine hushangaa ni nini ambalo Wakenya wanataka kwa sababu akiwapa mvua, wanalia na vile vile, akiwapa jua, bado wanalia. Ni kwa sababu sisi, kwa akili zetu duni, tumekataa kuona baraka ya Mungu na kuitumia halisi. Bi. Spika wa Muda, wakati wa mvua hatuhifadhi maji. Tunaacha maji yote yatiririke na kwenda baharini, halafu baadaye tunalia. Naunga mkono kabisa wale wenzangu ambao wamesema kwamba iwe ni sheria kwamba kila nyumba nchini, ambayo imejengwa kwa vifaa ambavyo vinaweza kuhifadhi maji, iwekwe tenki. Isiwe ni ombi bali ni sheria kwamba kila mtu anayeweza kujenga nyumba ambayo inaweza kumwaga maji awe na tenki la maji. Mpango kama huo utaondoa gharama sio tu kwa maji bali pia kuondoa maradhi. Hii ni kwa sababu maradhi mengi ambayo tunajua yanahusiswa kabisa na kunywa maji machafu. Maji ya mvua ambayo yamehifadhiwa huwa ni safi na hata gharama ya sabuni huwa kidogo kwa sababu maji ya mto hutumia sabuni zaidi wakati wa kufua nguo. Bi. Spika wa Muda, hata hivyo, ni lazima tuangalie sera za watu wazembe ambao kwa muda mrefu wametugharimu. Wakati wa Serikali iliyopita, wengine walijifanya kwamba wanachimba mabwawa kule Kitui na wakapewa pesa nyingi. Badala ya kuzitumia kuchimba mabwawa, walizitumia kwa ubinafsi. Haya mambo yamepita chini ya daraja na hatusikii Serikali ikifuatilia pesa hizo nyingi. Ni lazima tuwe na mabwawa sio tu katika tarafa bali hata vitongojini. Tunafaa kuwa na bwawa kila mahali ili maji ya mtiririko yaweze kuhifadhiwa kwa ajili ya kutumika wakati wa kiangazi. Tukifanya hivyo, hata uchumi wetu utakua kwa kasi na kuendelea, kwa sababu mwananchi atakuwa amepewa uwezo wa kukuza nafaka ambazo zinaweza kukuza uchumi vijijini, kwa mfano, nyanya na mboga. Pia, ng’ombe na kuku wanaweza kunywa maji mazuri, kwa sababu maji ni uhai. Iwapo wakulima wetu wanaweza kupata mapato kwa sababu ya uhifadhi bora wa maji, watoto wataenda shule na akina mama na baba watakuwa na afya nzuri kwa sababu ya kupata chakula kizuri. Maisha ya binadamu nchini Kenya yataongezeka na faida ya kuishi itakuwa nzuri. Bi. Spika wa Muda, kwa hivyo Hoja hii ni ya maana zaidi. Mikataba iliwekwa hapo awali kati ya mabeberu na Wakenya ya kushika maji yetu yote na kusema kuwa ni ya Misri. Mpaka sasa ni ukoloni mambo leo. Hayo tukatae lakini hata hivyo, tunatumia maji yaliyopo vipi? Ziwa Viktoria ambalo ni la pili kubwa zaidi ulimwenguni mzima lilikuwa na maji masafi. Je, ziwa hilo linatumika aje? Limekuwa ndio shimo la kupeleka uchafu wote wa hoteli na viwanda kwa miji yote inayozunguka ziwa hilo. Maji ya ziwa hilo na ya maziwa mengine katika Bonde la Ufa yakihifadhiwa na kutumiwa vizuri, yanaweza kusambazwa katika Kenya nzima. Lakini kwa sababu mipango yetu ni ya leo na sio kesho, hatuoni mbali. Tunaathirika, kuhangaika na kuteseka kwa jambo ambalo tunaweza kuepuka. Ni lazima tujipige moyo konde. Je, tulikosea wapi na mwelekeo ni upi? Wasomi, wapiga hesabu na viongozi tunao. Pia tuna pesa. Je, kama tuna nia, mipango bora na uwezo, shida ni nini? Ni uzembe tu; hakuna sababu nyingine. Kazi yetu ni kulalamika tu siku zote. Kwa hivyo, ni lazima tujenge mabwawa makubwa ya maji nyumbani, vijijini, vitongojini na hata katika nchi nzima kwa sababu maji ni uhai. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate."
}