GET /api/v0.1/hansard/entries/399428/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 399428,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/399428/?format=api",
"text_counter": 113,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Gathogo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 2715,
"legal_name": "Esther Nyambura Gathogo",
"slug": "esther-nyambura-gathogo"
},
"content": "Ahsante Bi. Naibu wa Spika. Nimesimama kuunga mkono Hoja hii. Sisi sote tunajua kwamba maji ni uhai. Wakati tuna maji mengi ni wakati mvua imenyesha. Maji humwagika kote kote hata barabarani. Hata hivyo kuna wakati kila mtu husumbuka. Kwa mfano, wafugaji husumbuka sana wakitafuta maji. Ikiwa tutachukua hatua ya kutafuta maji--- Watu wengi wanafikiria kwamba maeneo bunge ya mijini hayana shida ya maji. Ukweli ni kwamba maji yanahitajika katika kila maeneo bunge. Kila wakati watu wanalia kwamba mimea yao imekauka kwa sababu maji hayapo. Tukishikana mikono na tuhifadhi maji na tuyatumie vizuri, basi wakati wa kiangazi hatutakuwa na shida ya maji. Naunga mkono Hoja hii. Naomba serikali ifanye haraka ili wananchi wasaidike. Kuna wengi ambao wana shida zaidi ya wengine. Sisi sote tushikane mikono tuwaonyeshe wananchi jinsi ya kuhifadhi maji wakati tunapoyatumia. Ahsante sana."
}