GET /api/v0.1/hansard/entries/400594/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 400594,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/400594/?format=api",
"text_counter": 514,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Wario",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 252,
"legal_name": "Ali Wario",
"slug": "ali-wario"
},
"content": "Ahsante sana mhe. Spika. Nasimama kuchangia marekebisho ya Hoja yaliyoko mbele yetu. Tumetoa miezi sita kwa PIC. Kamati hii imeenda na ikatuletea Ripoti. Kwa masikitiko makubwa, imeamua kwamba kampuni fulani isipewe kazi na nyingine ipewe kazi. Baada ya sisi kusema kwamba hii ni kazi ya mahakama, tunaletewa marekebisho ili korti ikiamua kwa manufaa ya National Cereals and Produce Board (NCPB), jambo hili lifanyike. Swala nyeti ni moja. Je, korti itakapoamua kwamba Erad imeshinda, marekebisho haya yatakuwa na maana gani? Kwa nini tunapoteza muda wa Wakenya? Hii ni kwa sababu haya ni masuala ya mahakama."
}